Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Simba SC, John Bocco ameelezwa kupona
majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui FC na
muda wowote ataanza kucheza kama kocha atampanga.
Afisa habari wa Simba Haji Manara amethibitisha hilo wakati akijibu
maswali ya mashabiki wa klabu hiyo waliokuwa wanataka kujua hali ya
nahodha huyo wa Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram.
''Niwajuze tu kuwa hali ya Bocco anaendelea vizuri na yupo tayari
kucheza kama kocha atampanga'', Manara alimjibu moja ya mashabiki
waliouliza.
Aidha Manara ameongeza kuwa majeruhi pekee aliyebaki kwenye kikosi cha
Simba ni Haruna Niyonzima ambaye hivi karibuni alipelekwa India kwaajili
ya matibabu na Manara ameongeza kuwa naye yupo mbioni kurejea.
Majeruhi wengine wa muda mrefu ndani ya kikosi cha Simba ambao tayari
wameanza mazoezi mepesi ni mlinda mlango Said Nduda na mlinzi Salim
Mbonde ambao wote wamesajiliwa msimu huu wakitokea Mtibwa Sugar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni