Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo Jumanne Februari 27, 2018
limemtembelea mtunzi wa wimbo uliovuma zaidi miaka ya nyuma wa ‘Tanzania
yetu ndio nchi ya furaha’, Mzee Stephen Hizza ambaye anasumbuliwa na
ugonjwa wa saratani ya tezi dume.
Mzee Hizza amelazwa wiki chache zilizopita katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili wodi ya Kibasila Chumba Na.16 ameonekana afya yake
kuendelea vyema tofauti na kipindi cha nyuma kama ilivyoripotiwa awali
na vyombo vya habari.
Wimbo wa ‘Tanzania yetu ndio nchi ya furaha’ uliimbwa na Bendi ya
‘ Atomic Jazz Band’ miaka ya 19 70’s ikiongozwa na John Kijiko.
Jikumbushe wimbo huo hapa chini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni