Jumatano, 28 Februari 2018

Siku 100 toka Mwandishi wa Mwananchi achukuliwe na wasiojulikana




Leo February 28, 2018 Uongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) umefanya mkutano na waandishi wa habari na kuzungumza kuhusiana na mwandishi wa kampuni hiyo Azory Gwanda ambaye alipotea November 21, 2017.
Ikiwa zimepita siku 100 tangu mwandishi huyo amepotea, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Francis Nanai ameeleza kuwa kampuni hiyo imejitolea kuhudumia mahitaji ya familia ya mwandishi huyo.
Nanai ameeleza kuwa watalipia mahitaji ya watoto wa shule, bima ya afya, biashara ya kujikimu pamoja na gharama za chakula na kwamba kampuni itafanya hivi hadi pindi Bi Anna atakapoweza kusimama mwenyewe.
Taarifa zinaeleza kuwa wakati Azory anatekwa mkewe Anna Pinoni alikuwa mjamzito na alikuwa na mtoto wa miaka 6, Anna February 12, 2018 amejifungua mtoto wa kike waliyempa jina Gladness.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni