mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania
blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla
kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Mwenyekiti ccm Mkoa wa wa morogoro bi Doroth mwamsiku amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi ccm, mkoani morogoro kujenga umoja wa chama hicho na kuendelea kumuunga mkono mh rais Samia suluhu hassani pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuwaletea maendeleo watanzania.
Bi doroth ameyasema hayo akiwa ziara yake yakutembelea wanachama wa ccm katika halmashauri ya wilaya zote mkoani morogoro ,
ambapo akiwa katika kata ya mlimba june 2 ,2021 , halmashauri ya mlimba amehaidi kufuatilia kero ya wananchi wa mlimba ikiwemo ubovu wa barabara ifakara mlimba,na kero ya maji ambayo inawasumbua wakazi wa mji mdogo wa mlimba kwa miongo kadhaa licha ya kuwepo kwa mradi mkubwa wa maji ambao unasuasua,pamoja nakuhaidi kufuatilia mchakato wa kupewa mamlaka kamili ya mlimba kuwa wilaya inayojitegemea .
Aidha mwenyekiti huyo wa ccm ameongeza kuwa mara baada ya kukamilisha ziara hiyo atakwenda kuwaona baadhi ya wafanyabiashara wa mlimba ambao wapo mahabusu toka mwezi decemba 2020 ambao wanatuhumiwa kwa kesi ya uhujumu,mara baada ya kukutwa wakifanya shughuli za kilimo katika bonde la kilombero na makosa mengine ya utakatishaji wa fedha , ambapo pia ameowaomba wananchi waendeleee kutoa ushirikiano kwa mbunge wa jimbo la mlimba bwana godwin kunambi kwani ni mchapakazi,
Hata hivyo katika mkutano huo baadhi ya watendaji wa serikali ambao walieleza baadhi ya kero za wananchi wa kata ya mlimba na tarafa ya mlimba kwa ujumla .
Bi doroth mwamsiku pia amekabidhi vitendea kazi kwa makatibu kata wa chama cha ccm jimbo la mlimba rim paper zenye dhamani ya shilingi 390,000.
KESHO YETU INAANZA NA LEO: Lengo letu ni kurudisha mazingira kwa ajili ya kesho yetu iliyo njema zaidi.
Tunaadhimisha Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yenye kauli mbiu “Kurejesha Mfumo wa Ikolojia” kwa kupitia mkakati wetu wa #TigoGreenForKili tunarejesha (1
Safisha bahari & mitaa unamoishi
Rejeleza
Usitumie plastiki
Kula vyakula vinavyozalishwa kwa uendelevu
ziara ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi kwenye jimbo lake umekua na neema katika kata za Idete na Fumo baada ya mbunge huyo kuchangia Sh Milioni Sita kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya, Zahanati, Miundombinu ya Barabara na ujenzi wa Hosteli ya Sekondari Matundu Hill.
Akizungumza katika kata ya Idete ambayo wananchi wake walimueleza changamoto yao ya ujenzi wa kituo cha afya na hostel ya shule hiyo Mbunge huyo aliahidi kutoa Sh Milioni 2.8 kwenye kata hiyo ili ielekezwe kwenye ununuzi wa mifuko 50 kwa ajili ya kituo cha afya na mifuko mingine 50 ya ujenzi wa hostel hiyo huku akitoa Sh Laki Tatu ili inunue Projector ya kufundishia shuleni hapo.
Mbunge Kunambi amesema anafahamu umuhimu wa elimu ni mkubwa na yeye kama kiongozi ambaye anaunga mkono juhudi za serikali ya Rais Dk John Magufuli ya kutoa elimu bila malipo ana wajibu wa kuchangia ujenzi huo ili kuendelea kuzalisha kizazi cha wasomi nchini.
" Wakati wa kampeni nilipita na mkanieleza shida zenu, nimekuja hapa ili tuanze na zile changamoto kubwa kwetu lakini lengo letu ni ndani ya miaka mitano hii mliyotupa dhamana kuhakikisha tunakamilisha kwa kiasi kikubwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama ambavyo ilituelekeza," Amesema Mbunge Kunambi akiwa katika kata ya Idete.
Amesema hii ni ziara yake ya kwanza tangu aapishwe kuwa Mbunge na mpaka sasa ameshatembelea kata 11 kati ya 16 zilizopo kwenye jimbo lake huku akitatua changamoto mbalimbali kwenye kata zote alizozitembelea.
" Ziara yangu ina sura mbili moja ni kuwashukuru kwa kumchagua kwa kishindo Rais wetu Dk Magufuli, mimi mbunge wenu na madiwani wa CCM, tulianzia Kata ya Uchindile na bado tuna kata tano ili tuhitimishe kata zote 16, lakini sura ya pili ni kuanza kutatua changamoto na kero zetu, niwaahidi zipo ambazo tutazimaliza ndani ya mwezi mmoja, zipo tutakazochukua mwaka mzima na zipo ambazo tutazimaliza ndani ya miaka mitano, lakini niwahakikishie hatutoacha sehemu," Amesema Mbunge Kunambi.
Akiwa katika kata ya Fomu, Kunambi pia amechangia Sh Milioni 3.5 ili zielekezwe kwenye kumalizia boma la ujenzi wa kituo cha afya pamoja na kusaidia kivuko cha awali kwenye barabara ya kata hiyo ili wananchi waweze kupata bila kupata shida.
Akizungumza baada ya mchango ya mbunge huyo mmoja wa wanufaikaji ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya matundu Hills Kasmiri Stephano amempongeza Mbunge huyo kwa jitihada zake hizo huku akisema zitasaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hasa wa kike ambao watakua wakikaa kwenye hostel hizo huku akimuomba kuzidi kuiangalie shule hiyo.
" Namshukuru sana Mbunge wetu, kumalizia ujenzi wa hostel yetu kutakua ni msaada kwetu sisi wanafunzi wa kike lakini pia ametoa fedha za kununulia projector kitu ambacho tunaamini kitakua ni msaada kwa walimu wetu katika kutufundishia," Amesema mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo.
1. The Sourtoe Cocktail
Hicho ni kinywaji kinachopatikana katika Jiji la Dawson, Canada, maeneo
ya Yukon. Kinywaji hicho huwa kina kidole cha mguu wa binadamu ndani
yake ambacho kimekolezwa chumvi. Kiuhalisia, hutakiwi kukila kidole
hicho, japokuwa wengine huvila kwa bahati mbaya. Lakini wakati
unamalizia kinywaji hicho kwenye bilauri, ni dhahiri kidole hicho
kitagusa midomo yako!
2. Snake Wine
Hiyo ni divai (wine) inayopatikana nchini Vietnam, ambayo ndani yake
huwekwa nyoka wazima, wakabakia humo wakiwa wazima au wamekufa.
Wanywaji wasioogopa, hunywa divai hiyo na kuwala nyoka hao.
3. Seagull Wine
Hii ni divai inayotumiwa na Waeskimo ambapo ndani yake hutumbukizwa
ndege wa baharini aliyekufa kwa ajili ya kuikoleza. Kwa hiyo, wanywaji
huamua wenyewe matumizi ya ndege huyo.
4. Lizard Wine
Hii ni divai inayotokana na mchele ambayo inatumiwa nchini China. Ndani
yake hujazwa mijusi ambapo mchanganyiko huo hudaiwa kumlinda mnywaji
dhidi ya mapepo mabaya.
5. Chicha de Muko
Hii ni pombe ya mahindi ambayo kutayarishwa kwake ni pamoja na
kuyatafuna mahindi na kisha kuyatemea kwenye chombo maalum ambamo
huwekwa na kuchanganywa na vitu vingine hadi inakuwa pombe.
6. Kumis (Fermented Mare’s Milk)
Hii ni pombe itokanayo na maziwa ya farasi yaliyowekwa hadi yakachachuka, inatumiwa na watu wa Mongolia.
7. Yak Butter Tea
Hii ni chai inayotumiwa huko Tibet ikiwa ni mchanganyiko wa siagi,
majani ya chai na chumvi ambavyo huongezewa ngano iliyokaangwa na maziwa
ya mtindi.
8. Bilk (Milk Beer)
Hii ni bia inayotumiwa nchini Japan ikiwa ni mchanganyiko wa maziwa, shayiri na mimea ya mihopi (hop).
9. The Aunt Roberta cocktail
Hiki ni kinywaji cha mchanganyiko wa gin, vodka, brandy, matunda aina
ya absinthe na blackberry. Kinatumika pia kusafishia vyombo ikiwa ni
pamoja na kudeki sakafu.
Chama cha Soka Barani Ulaya (UEFA) kimesema kipo kwenye hatua za
mwisho kuja na michuano mipya kwa ngazi ya vilabu barani humo, ambayo
itakuwa ni michuano ya tatu kwa ukubwa baada ya #UEFAChampionsLeague na #EuropaLeague.
Mkuu wa Chama cha Vilabu barani Ulaya (ECA) Andrea Agnelli ndiye
aliyetoa taarifa hiyo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho
unaofanyika nchini Croatia, lakini hajaweka wazi mfumo wa mashindano
hayo utakavyokuwa.
Pichani ni Benjamani Mkapa akila kiapo Cha Kuwa Balozi wa Tanzania
Nchini Nigeria Mbele ya Rais Julius Kambarage Nyerere IKULU Jijini Dar
Tarehe 18-10-1976,Katikati ni Katibu wa Rais Wakati huo Ndugu Timothy
Opiyo.
Miaka
17 imepita tangu dunia ilipotingishika kufuatia mashambulizi makubwa ya
kigaidi yaliyolenga jengo refu zaidi duniani, World Trade Centre jijini
New York na Jengo la Wizara ya Ulinzi (Pentagon) jijini Washington. Leo
Wamarekani wakiongozwa na Rais Donald Trump, wataadhimisha kumbukumbu
ya tukio hilo lililotokea Septemba 11, 2001 ambapo zaidi ya watu 3000
walipoteza maisha, shughuli itakayofanyika Shanksville, Pennsylvania
nchini humo. Japokuwa
siku nyingi zimepita, bado jinamizi la tukio hilo linaendelea
kuwasumbua Wamarekani wengi, hasa wale waliopoteza ndugu zao kwenye
tukio hilo baya zaidi katika historia ya ugaidi duniani huku wengine
wakiachwa na ulemavu wa kudumu. Katika
maadhimisho hayo, watu wote watasimama kimya kwa dakika moja kuwaenzi
wote waliopoteza maisha katika tukio hilo, huku majina ya watu wote
waliopoteza maisha yakitajwa. Wamarekani
wengi wameendelea kuisisitiza serikali yao kuhakikisha tukio kama hilo
halijirudii ndani ya ardhi ya nchi hiyo na kufanya kila kinachowezekana
kukomesha ugaidi duniani kote.
Mshukiwa
mkuu wa matukio hayo, Osama bin Laden aliyekuwa kiongozi wa Kundi la Al
Qaeda, aliuawa Mei 2, 2011 Abbottabad, Pakistan na majeshi ya Marekani
chini ya Rais Barrack Obama, katika oparesheni iliyopewa jina la
Neptune Spear.
Mwenyekiti
waBaraz la wazee Chadema Bw. Hashimu Juma amedai kuwa chadema na CUF ni
kitu kimoja hivyo basi kama CCM wakifanikiwa kumtoa maalim seif
zanzibar basi kutokana na wao kuwa kitu kimoja maalimu atachukua fomu
kupitia chama hiko cha chadema pamoja na viongozi wengine wote wa maalim
seif.
Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya
England Luke Shaw aliyepata mshtuko baada ya mgongano wa bahati mbaya na
beki wa Uhispania Dani Carvajal katika nusu ya pili ya mchezo
uliowakutanisha miamba hao wawili ambapo England akiwa nyumbani
alifungwa goli 2-1 na Hispania
Baada ya majeraha hayo ya kichwa Shaw alirudi United kwa ajili ya
ufuatiliaji zaidi na matibabu siku ya Jumatatu licha ya beki huyo kuumia
wakati anaitumikia timu yake ya taifa.
akiongea na wanahabari kocha wa timu ya taifa ya England Gareth
Southgate alisema ” Hakuna mtu aliyetamani kuona tukio kama hilo”na
kuongeza kuwa Shaw alitolewa uwanjani akiwa amefungwa vifaa vya
kumuingizia hewa ya oksijeni lakini alisema kuwa amepata tena ufahamu
haraka katika chumba cha matibabu, na hivi karibuni alikuwa akiwasiliana
na marafiki na familia.
Baada ya beki huyo kisiki mwenye ustadi wa aina yake kuumia katika
mchezo huo wa jumamosi dhidi ya Uhispani huku kocha wake Jose Mourinho
akishuhudia jukwaani, msaada wa beki huyo utakosekana katika timu yake
ya Manchester United katika mchezo wao wa siku ya jumamosi dhidi ya
Watford,hivyo Luke Shaw hatakuwepo kwenye mchezo huo utakaofanyika
katika dimba linalomilikiwa na The Golden Boys au jeshi la njano Watford
linalojulikana kama Vicarage Road Stadium.
Siku chache kabla, Shaw alikuwa amefungua hadithi ya hofu ya mguu wake
uliovunjika, ambalo alikiri alikuwa karibu na kumchukuliwa na
kumlazimisha kufikiria kustaafu kutoka mchezo huo kwa umri wa miaka 23
tu.