Jumamosi, 2 Desemba 2017

Mambo Ambayo Unatakiwa Kuyakumbuka Kila Wakati


 Naomba pia nitumie wasaha huu kuweza kukaribisha katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza juu ya mafanikio. Naamini unajua kujifunza hakuna mwisho, hivyo unatakiwa kila siku kuweka maarifa ya kukusaidia, ukishindwa kufanya hivyo utakwama.

Katika makala yetu ya leo nitaomba tu nikukumbushe mambo ambayo unatakiwa uyakumbuke kila wakati kwenye  maisha yako . Ni mambo ya msingi kwani yatakusaidia kuweza kuwa na mtazamo chanya na kubadili mambo mengi sana kwako.

1. Mambo yaliyopita hayawezi kubadilishwa tena.
Unatakiwa kuelewa kama kuna mambo ambayo yameshapita huwezi kuyabadilisha tena hata kama yalikuumiza au ulifanya makosa kiasi gani. Kwa sasa unatakiwa kuganga yajayo, habari ya mambo yaliyopita yatumie kama fundisho tu kwako, lakini ndio yameshapita, usiumize kichwa na kujilaumu sana.

2. Maoni ya watu hayaamui hatima ya maisha yako.
Hata siku moja usije ukakaa ukafikiri kwamba maoni ya watu wengine wanayosema juu ya wewe ndiyo yanaamua maisha yako yawe vipi. Maisha yako yanabaki hivyo yalivyo kwa sababu wewe umeamua yawe hivyo. Lakini usikubali hata siku moja maoni ya watu yakurudishe nyuma na usiyatumie kama kisingizio.

3. Maisha yako yatakuwa mazuri tu ukijipa muda.
Ukiamua siku zote kubadilisha maisha yako unaweza. Kikubwa jipe muda wa kutosha kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua na kila kitu kitabadalika. Haijalishi unaona maisha yako ni magumu kiasi gani, lakini muda ndio kila kitu. Muda unaweza kusawazisha mambo mabaya na yakawa mazuri kabisa. Tumia muda wako vizuri.

4. Utashindwa tu, kama utakata tamaa.
Ndoto yoyote ile uliyonayo au ambayo unatamani kuifikia una uwezo mkubwa wa kuifikia. Ila hautaweza kuifikia ndoto yako hiyo ikiwa utafika mahali wewe mwenyewe utaamua kukata tamaa. Moja ya sumu kubwa ya kimafanikio ni kukata tamaa, ukikata tamaa ujue kila kitu kwako kimeishia hapo na hutaweza kusogea tena.

5. Furaha ya kweli inapatikana ndani mwako.
Ukweli huu hautakaa ubadilike kamwe kwamba furaha ya kweli inapatikana ndani mwako na wala si nje yako. Unaweza ukakazana sana kutafuta furaha nje kwa kufanya vitu ambavyo unaamini vitakupa furaha, lakini ukivipata vitu hivyo unashangaa ile furaha tena bado huna. Hivyo jifunze kutafuta furaha ya kweli ndani mwako.

6. Mawazo chanya, ni njia ya mabadiliko chanya pia.
Mbinu mojawapo ya kuwa na maisha bora. Ni kwa wewe kuwa na mawazo chanya. Unapokuwa na mawazo chanya ni rahisi sana kwa wewe kuweza kuleta mabadiliko chanya pia. Watu wengi wanashindwa kwa sababu ya kuwa na mlundikano wa mawazo mengi ambayo kwao ni hasi. Kuwa na mawazo chanya ubadili maisha yako.

Yapo mambo mengi ya kukumbuka kila unapoelekea kwenye mafanikio yako. Kwa leo hii nimekukumbusha mambo haya machache. Kwa kuyafanyia kazi itakuwa sehemu kubwa ya mabadiliko kwenye maisha yako.

Ijumaa, 1 Desemba 2017

Nyalandu: Ni uzalilishaji mkubwa unaoendelea Libya




Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa wa Singida Kaskazini aliyejiuzulu, Lazaro Nyalandu ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua zaidi juu ya kinachoendelea nchini Libya.

Amesema kuwa ni lazima hatua zichukuliwe kwa kile kinachoendelea nchini Libya ili kuweza kukomesha kile ambacho kinaendelea kwa sasa dhidi ya binadamu.

“Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika lazima uchukue hatua dhidi ya Libya sasa. tunachoshuhudia ni matusi kwa wanadamu,”amesema Nyalandu

Aidha, siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zikiripotiwa kutoka Libya kuwa kumekuwa na biashara ya utumwa ikifanyika ikihusisha Libya kuuza Waafrika nchi za Ulaya.

Ubalozi wa Libya nchini Tanzani umesema kuwa Waafrika wanaodaiwa kuuzwa kutoka nchi hiyo, yawezekana walikuwa wanakabidhiwa kwa watoroshaji ili wawapeleke Ulaya na sio kuwauza kama watumwa.

TFF yamjibu Zitto Kabwe




Shirikisho la Soka Tanzania TFF limejibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuitaka Tanzania isusie kucheza mechi na Libya ili kupinga vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea nchini humo.

Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa suala hilo ni nyeti na limefikishwa katika uongozi wa juu na kwamba litatolewa majibu hivi karibuni.

“Msimamo utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa,” amesema Lucas

Jana, Zitto alitoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilimanjaro Stars isusie mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biashara ya utumwa.

Wakuu wa jeshi wateuliwa kuwa mawaziri Zimbabwe

Rais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri


Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelitaja baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu katika serikali yake.
Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo , jenerali aliyetangaza katika runinga ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti.
Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri ataongoza wizara ya fedha na kilimo.
Kiongozi mmoja wa upinzani Tendai Biti amesema kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.


Bwana Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliopita kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban miaka saba.
Upinzani umelaumu mabadiliko hayo kama usaliti wa matumaini miongoni mwa raia na thibitisho kuwa vikosi vya usalama vilivyokuwa na nguvu nyingi wakati wa utawala wa Mugabe vinaendelea kuthibiti taifa hilo.
Hali ya kuleta uwiano na umoja ilioonekana katika siku za karibuni huenda ikabadilishwa na makabiliano ya uongozi katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Harufu mbaya ya soksi yamtia abiria matatani India

Picha ya kuashiria


Polisi nchini India wanasema wamemkamata mwanamume mmoja ambaye uvundo wa soksi zake ulisababisha ugomvi kati yake na abiria wenzake kwenye basi.
Waliambia BBC kwamba wamewasilisha kesi dhidi ya Prakash Kumar, 27, kwa "kuvuruga amani ya umma".
Kisa hicho kilitokea kwenye basi lililokuwa safariki kuelekea mji mkuu Delhi, baada ya Kumar kuvua viatu vyake na soksi.
Harufu mbaya kutoka kwenye soksi zake ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba abiria walimuomba Bw Kumaru kuziweka ndani ya mkoba wake au kuzirusha nje ya basi.
Lakini anadaiwa kukataa hilo, na ugomvi mkali ukazuka.
Abiria kisha walimlazimisha dereva wa basi hilo kuingia kituo cha polisi katika jimbo la Himachal Pradesh, kaskazini mwa India, ambapo malalamishi dhidi yake yaliwasilishwa.


Gazeti la Hindustan Times limemnukuu Bw Kumar akisema kwamba soksi zake hazikuwa na harufu mbaya, na kwamba abiria wenzake waligombana naye "bila sababu".
Polisi wameambia BBC kwamba mwanamume huyo amepewa dhamana.

Mila za kichaga kuanza kuchunguzwa na TAKUKURU






Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Hai mkoani Kilimanjaro (Takukuru), imeanza kuchunguza utamaduni wa familia za kabila la Wachaga za kutumia majani kufunika au kumaliza kienyeji kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia na mimba za wanafunzi.




Tokeo la picha la TAKUKURU



Majani hayo maarufu kwa jina la Sale/Masale kwa mila na tamaduni za kabila la Wachaga, hutumika kuashiria amani, kuomba msamaha na kumaliza tofauti zao na mara nyingi hutumika pale kunapokuwa na matatizo baina ya pande mbili.
Ofisa wa Takukuru Wilaya ya humo, Denis Mazigo amefichua siri hiyo ya kuanza kwa uchunguzi dhidi ya mila hiyo wakati wa uwasilishaji ripoti ya Kamati ya Ulinzi wa Mtoto.
“Haliwezi kutangulizwa jani la sale peke yake, lazima kuna mazingira ya kutolewa kwa fedha kama rushwa, ndiyo msamaha uweze kukubalika. Sasa sisi kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa tumeanza kufanyia kazi jambo hili, kwa sababu tumeona kesi nyingi za ukatili zikikwama huku zikiwa na ushahidi wa kutosha.” amesema Mazigo.
Chanzo : Nipashe

Umeme wakatika karibia nchi nzima kuanzia jana






Dar es Salaam. Wakati umeme ukiwa umekatika nchi nzima kuanzia jana Alhamis, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema huduma hiyo imeanza kurejea kwenye mikoa ya Iringa, Dodoma na Tanga.

Akizungumza leo Ijumaa, Desema 1, 2017, Kaimu Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Leila Mhaji amesema umeme umekatika katika mikoa yote iliyounganishwa katika gridi ya Taifa.

Amesema wataalam wa shirika hilo wanaendelea kurekebisha mifumo ya gridi ya Taifa ili kufanya matengenezo ya hitilafu iliyotokea.

“Marekebisho ya mafundi wetu yamesababisha umeme kurejea katika mikoa ya Iringa, Dodoma na Tanga,” amesema.

Amesema wataalam wamegundua mfumo wa gridi haujatengemaa vizuri na hivyo wanaendelea na kazi ya kurekebisha usiku na mchana ili kuhakikisha huduma hiyo inarejea katika hali yake ya kawaida.

“Tutaendelea kuwapa taarifa na tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza,” amesema.

Amewatahadharisha wananchi kutokushika wala kukanyaga nyaya zilizokatika au kuanguka kwa kuwa ni hatari.

Ameitaja mikoa ambayo umeme haujakatika kuwa ni Kagera na Ruvuma ambayo haijaunganishwa na gridi ya Taifa.

IGP Siro, RC Makonda, Mo Dewji, Dkt. Kigwangala kuunda kamati AFCON U17



 Ukiacha Kamati Kuu ya kuratibu michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U17/2019) kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya uteuzi mwingine.

Uteuzi huo umeegemea zaidi kwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Maandalizi (LOC) wakiwamo viongozi wakuu wa TFF na wanafamilia wengine ambao kwa pamoja watafanya kazi ya kuandaa michuano hiyo itakayofanyika Tanzania mwaka 2019.
Wakati jina namba moja ni Mwenyekiti wa kila kamati ndogo wajumbe wengine katika kamati hizo ni kama ifuatavyo:
Miundombinu (Infrastructure)
  1. 1. Paul Makonda (Mwenyekiti)
  2. 2. Yusuph Singo
  3. 3. Sunday Kayuni
  4. 4. Leslie Liunda
  5. 5. Nassoro Idrissa
  6. 6. Mohamed Kiganja
  7. 7. Mhandisi Davis Shemangale

Masoko na Habari (Marketing, Commercial and Media)
  1. 1. Kelvin Twissa (Mwenyekiti)
  2. 2. Angetile Osiah
  3. 3. Dk. Hassan Abbas
  4. 4. Dk. Omari Swaleh (Chuo Kikuu cha Mzumbe)
  5. 5. Iman Kajula
  6. 6. Tido Mhando
  7. 7. Head of Marketing – NMB
Fedha na Mipango (Finance and Planning)
  1. 1. Doto James (Mwenyekiti)
  2. 2. Mohamed Dewji
  3. 3. Dk. Seif Muba
  4. 4. Bernard Lubogo
  5. 5. Paul Bilabaye
  6. 6. Jacquelline Woiso
  7. 7. Cornel Barnabas
Usafiri na Malazi (Transport and Accommodation)
  1. 1. Mhandisi Ladislaus Matindi (Mwenyekiti)
  2. 2. Abubakar Bakhresa
  3. 3. Aziz Abood
  4. 4. Alhaj. Ahmed Mgoyi
  5. 5. Mhe. Ahmed Shabiby
  6. 6. Dk. Maige Mwakasege Mwasimba
  7. 7. Shebe Machumani
Uratibu Utalii
  1. 1. Dkt. Khamis Kigwangala (Mwenyekiti)
  2. 2. Allan Kijazi
  3. 3. Devotha Mdachi
  4. 4. Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke
  5. 5. Hoyce Temu
  6. 6. Leah Kihumbi (Mkurugenzi Sanaa)
  7. 7. Athuman Jumanne Nyamlani
Itifaki
  1. 1. Kamishna Mkuu wa Uhamiaji (Mwenyekiti)
  2. 2. Mndolwa Yusuph
  3. 3. Filbert Bayi
  4. 4. Mkurugenzi Uwanja wa Ndege JNIA
  5. 5. Happiness Luangisa
  6. 6. Alex Makoye Nkenyenge
  7. 7. Alhaji Idd Mshangama
Tiba na Udhibiti wa Dawa za Kusisimua Misuli (Medical and Doping Control)
  1. 1. Prof. Lawrence Museru (Mwenyekiti)
  2. 2. Dkt. Paul Marealle
  3. 3. Dkt. Edmund Ndalama
  4. 4. Dkt. Christina Luambano
  5. 5. Daktari Mkuu wa Hospitali ya Temeke
  6. 6. Hiiti Sillo
Sheria na Taratibu
  1. 1. William Erio (Mwenyekiti)
  2. 2. Dk. Damas Ndumbaro
  3. 3. Edwin Kidifu
  4. 4. Ally Mayai
  5. 5. Khalid Abeid
Ulinzi na Usalama (Safety and Security)
  1. 1. IGP. Simon Siro (Mwenyekiti)
  2. 2. Michael Wambura
  3. 3. CP. Andengenye – Zimamoto
  4. 4. CP. Lazaro Mambosasa – Polisi Kanda ya Dar-es-Salaam
  5. 5. Mkuu wa Askari wa Usalama Barabarani.
  6. 6. TISS
  7. 7. Jonas Mahanga
Rasilimali Watu (Human Resources)
  1. 1. Dk. Francis Michael (Mwenyekiti)
  2. 2. Allan Kijazi
  3. 3. Wane Mkisi
  4. 4. Juliana Yassoda
  5. 5. Gerald Mwanilwa
Kamati hizo ndogo zitakuwa chini ya Kamati Kuu inayoongozwa na Mwenyekiti Dk. Harrison Mwakyembe (MP); Makamu Mwenyekiti wa Leodegar Tenga na Mtendaji Mkuu wa Kamati hiyo ni Henry B. Tandau.

Kamusoko azua mtafaruku Yanga




SIKU chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari wa Tiba za Michezo Tanzania (Tasma), Nasoro Matuyza kutangaza kuomba wadau wamchangie kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko raia wa Zimbabwe, kumezua mtafaruku wa aina yake.
Matuzya ambaye amewahi kuwa daktari wa Yanga mara kadhaa alitoa taarifa ya maombi hayo mtandaoni na kueleza kuwa Kamusoko ana tatizo kubwa la goti lakini anawe­za kumsaidia endapo kiwango fulani cha fedha kitapatikana.
Alisema kufanikisha mati­babu ya Kamusoko, inahitajika Sh 720,000 ili kutibu tatizo la kupasuka kwa kikombe cha ndani cha mguu wa kushoto akitolea mchanganuoa wa fedha hiyo alisema Sh 480,000 kwa kipimo cha MRI, Sh 158, 000 dawa na vifaa tiba na Sh 82,000 ya X Ray, Ultra Sonic Sound pamoja na kumuona daktari.
Akizungumza juu ya kilichotokea baadaye alisema: “Nimeamua kuachana na Kamusoko hadi hapo baadaye uongozi utakaponikabidhi, nilitoa taarifa ile kwa nia njema lakini kuna watu wameni­shambulia na kuniona natafuta fedha kinguvu.”
Alipotafutwa Daktari wa Yanga, Edward Bavo alisema: “Hizo taarifa za mitandaoni mimi sizipen­di, Kamusoko yuko fiti na alikuwa aanze mazoezi lakini kwa kuwa ligi imesimama, ataanza pamoja na wenzake, sijaonana naye kwa siku kadhaa, sijui chochote kuhusu taarifa za Matuzya unazoniam­bia.”
Walipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa na Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten hawakupatikana.

Kikosi cha Simba chabadili ratiba




Vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2017/18 Simba SC, imebadili ratiba yake ya kuanza mazoezi baada ya kuwapa mapumziko wachezaji wake kufuatia kusimama kwa ligi.
Kikosi cha Simba SC sasa kitaanza mazoezi yake rasmi siku ya Jumatatu kwenye viwanja vya Polisi Jijini Dar es Salaam. Awali taarifa ya klabu ilieleza kuwa timu ingeanza mazoezi ijumaa hii.
Simba itakuwa inajiandaa na mchezo wake wa raundi ya 12 ligi kuu soka Tanzania Bara, ambapo itakuwa mgeni wa Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) imesimama kwa muda kupisha michuano ya kombe la CECAFA Challenge inayotarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu.

leo ni siku ya ukimwi duniani

Image result for vvu images

 Ikiwa leo ni siku ya Ukimwi duniani, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza harakati dhidi ya Ukimwi, UNAIDS imeonyesha kuwa wanaume ni wagumu zaidi kukubali kupima Virusi Vya Ukimwi, kuliko wanawake.





 Huyu ni Mpho Tlabaki mkazi wa Lesotho akitoa ushuhuda wa ugumu wa wanaume kukubali kupima virusi vya ukimwi, VVU.





 Niligundua kuwa wanaume wanakosa uelewa kuhusu afya kwasababu kwa upande wangu nilipima mara mbili nikakutwa nina VVU lakini sikuamini. Kwa ujumla wanaume hawana uelewa na wengi wao wanasaka ushauri kwa waganga wa kienyeji badala ya kwenda hospitali."
UNAIDS inasema pamoja na kukosa uelewa, wanaume pia ni wagumu kufuatilia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi na pia wako hatarini zaidi kufariki dunia kutokana na Ukimwi kuliko wanawake.


Katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara, wanawake na wasichana wako tayari mara 60 zaidi kufahamu hali yao kuhusu Ukimwi kuliko wanaume na wavulana.
Tayari serikali ya Lesotho imewezesha uwepo wa wauguzi wanaofuata wagonjwa majumbani ikiwemo Mpho ili kufuatilia matumizi ya dawa.

MAGAZETI YA LEO 1/12/2017