Ijumaa, 1 Desemba 2017

leo ni siku ya ukimwi duniani

Image result for vvu images

 Ikiwa leo ni siku ya Ukimwi duniani, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza harakati dhidi ya Ukimwi, UNAIDS imeonyesha kuwa wanaume ni wagumu zaidi kukubali kupima Virusi Vya Ukimwi, kuliko wanawake.





 Huyu ni Mpho Tlabaki mkazi wa Lesotho akitoa ushuhuda wa ugumu wa wanaume kukubali kupima virusi vya ukimwi, VVU.





 Niligundua kuwa wanaume wanakosa uelewa kuhusu afya kwasababu kwa upande wangu nilipima mara mbili nikakutwa nina VVU lakini sikuamini. Kwa ujumla wanaume hawana uelewa na wengi wao wanasaka ushauri kwa waganga wa kienyeji badala ya kwenda hospitali."
UNAIDS inasema pamoja na kukosa uelewa, wanaume pia ni wagumu kufuatilia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi na pia wako hatarini zaidi kufariki dunia kutokana na Ukimwi kuliko wanawake.


Katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara, wanawake na wasichana wako tayari mara 60 zaidi kufahamu hali yao kuhusu Ukimwi kuliko wanaume na wavulana.
Tayari serikali ya Lesotho imewezesha uwepo wa wauguzi wanaofuata wagonjwa majumbani ikiwemo Mpho ili kufuatilia matumizi ya dawa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni