
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2017/18 Simba SC,
imebadili ratiba yake ya kuanza mazoezi baada ya kuwapa mapumziko
wachezaji wake kufuatia kusimama kwa ligi.
Kikosi cha Simba SC sasa kitaanza mazoezi yake rasmi siku ya Jumatatu
kwenye viwanja vya Polisi Jijini Dar es Salaam. Awali taarifa ya klabu
ilieleza kuwa timu ingeanza mazoezi ijumaa hii.
Simba itakuwa inajiandaa na mchezo wake wa raundi ya 12 ligi kuu soka
Tanzania Bara, ambapo itakuwa mgeni wa Ndanda FC kwenye uwanja wa
Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) imesimama kwa muda kupisha michuano ya
kombe la CECAFA Challenge inayotarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17 mwaka
huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni