
SIKU chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari wa Tiba za
Michezo Tanzania (Tasma), Nasoro Matuyza kutangaza kuomba wadau
wamchangie kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko raia wa Zimbabwe, kumezua
mtafaruku wa aina yake.
Matuzya ambaye amewahi kuwa daktari wa Yanga mara kadhaa alitoa taarifa
ya maombi hayo mtandaoni na kueleza kuwa Kamusoko ana tatizo kubwa la
goti lakini anaweza kumsaidia endapo kiwango fulani cha fedha
kitapatikana.
Alisema kufanikisha matibabu ya Kamusoko, inahitajika Sh 720,000 ili
kutibu tatizo la kupasuka kwa kikombe cha ndani cha mguu wa kushoto
akitolea mchanganuoa wa fedha hiyo alisema Sh 480,000 kwa kipimo cha
MRI, Sh 158, 000 dawa na vifaa tiba na Sh 82,000 ya X Ray, Ultra Sonic
Sound pamoja na kumuona daktari.
Akizungumza juu ya kilichotokea baadaye alisema: “Nimeamua kuachana na
Kamusoko hadi hapo baadaye uongozi utakaponikabidhi, nilitoa taarifa ile
kwa nia njema lakini kuna watu wamenishambulia na kuniona natafuta
fedha kinguvu.”
Alipotafutwa Daktari wa Yanga, Edward Bavo alisema: “Hizo taarifa za
mitandaoni mimi sizipendi, Kamusoko yuko fiti na alikuwa aanze mazoezi
lakini kwa kuwa ligi imesimama, ataanza pamoja na wenzake, sijaonana
naye kwa siku kadhaa, sijui chochote kuhusu taarifa za Matuzya
unazoniambia.”
Walipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa na Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten hawakupatikana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni