
Shirikisho
la Soka Tanzania TFF limejibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma
Mjini Zitto Kabwe, kuitaka Tanzania isusie kucheza mechi na Libya ili
kupinga vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea nchini humo.
Afisa
habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa suala hilo ni nyeti na
limefikishwa katika uongozi wa juu na kwamba litatolewa majibu hivi
karibuni.
“Msimamo
utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali
halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa
juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa,” amesema Lucas
Jana,
Zitto alitoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilimanjaro Stars isusie
mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na
vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biashara ya
utumwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni