Jumamosi, 8 Julai 2017

Nay wa Mitego ni sawa na Gigy Money na Amber Lulu! – Dudu Baya



 Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Dudu Baya amedai muziki wa rapa Nay wa Mitego hautofautiani sana na muziki wa Gigy Money na Amber Lulu huku akidai ni muziki uliotawaliwa na majungu na majigambo.

, Dudu amewashangaa mashabiki wa muziki kuendelea kumpatia support rapa huyo wakati haoni chochote anachofanya kwenye muziki.
“Mimi sio shabiki wa muziki wa Nay wa Mitego, kwanza muziki wake haueleweki ndio maana namfananisha na Amber Lulu na Gigy Money,” alisema Dudu Baya. “Kuna wasanii wakali wanafanya muziki mzuri kuliko huyo lakini hawapewi support, mimi ningewashauri tu mashabiki wa muziki wapende muziki mzuri,”
Alisema hajui rapa huyo anafanya muziki wa namna gani kwani amekuwa ni msanii wa hip hop anayetumia mwamvuli wa hip hip kuwasema watu.
Rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki kusikiliza muziki mzuri ambao utawajenga na sio muziki ambao ndani yake una maneno ya kuwasema watu bila sababu.
chanzo bongo 5.

Taifa Stars wamepata nafasi ya mshindi wa tatu vs Lesotho



 
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars jana July 7 2017 imefanikiwa kuingia kwenye headlines baada ya kupata ushindi katika game ya michuano ya COSAFA ya kutafuta mshindi wa tatu iliyochezwa Afrika Kusini. Taifa Stars game ya kutafuta mshindi wa tatu imecheza dhidi ya timu ya taifa ya Lesotho na dakika 90 zikamaliza kwa sare tasa (0-0) kutokana na timu hizo kutoshana nguvu na kila moja kufanikiwa kumiliki mpira kwa asilimia 50 ndio mikwaju ya penati ikaamua mshindi.




Licha ya Lesotho kuonekana kuwa wazuri kiasi na kufika golini kwa Taifa Stars mara nyingi lakinihawakuwa wazuri katika upigaji penati na wakajikuta wakifungwa kwa penati 4-2, huku kwa upande wa Tanzania Shiza Kichuya ndio alikosa penati, Himid Maoa, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Alpha wakafunga penati zote.

Ommy Dimpoz atuhumiwa kuiba Wimbo




Producer wa muziki bongo Abydad amedai kudhulumiwa wimbo aliokuwa amemuandalia msanii wake kisha kupatiwa msanii Ommy Dimpoz ambaye  siku ya jana ameuachia rasmi  ulichukuliwa na mtayarishaji Lolli Pop (GoodLuck Gozbert) kwa ajili ya kuuboresha.
Akizungumza leo kwenye kipindi cha Planet Bongo Abydad amesema kwamba ameshtushwa sana kuusikia wimbo mpya wa Ommy Dimpoz kwani yeye na msanii wake walikuwa katika hatua za mwisho za kufanya video baada ya Loly Pop kuanza kumpiga kalenda kurudisha wimbo aliodai anaenda kuufanyia maboresho.
 
 Hii ni project yangu ambayo niliifanya na msanii wangu mchanga anayeitwa Modala tangu Januari mwaka jana. Wakati naiandaa Lolli Pop alikuwa studio na yeye alishauri kwamba tumsaidie mdogo wetu atoke, kwa hiyo huu wimbo tuuboreshe vitu na kwa vile sisi tuna tabia ya kushirikiana sikuona shida kumpatia kwa kuwa nilimuamini sasa nilikuja kushtuka baada ya jana kuusikia Ommy anautambulisha alafu anasema kaandikiwa na Lolli Pop" Abydad alifunguka.
Mwanamuziki na Mtayarishaji wa muziki Lolli Pop (Goodluck Gozbert)
Pamoja na hayo Abydad amesema kwamba hataweza kuchukua hatua zozote kwa ajili ya kitendo hicho bali amewaaonya watu wote wenye tabia za aina hiyo waweze kuziacha kwani kunaua vipaji vya vijana wenye ndoto za kufikia mafanikio kama waliyonayo wa
chanzo na muungwana blog.

Tupac alidai Madonna alivunja uhusiano wao kwa sababu ya ubaguzi


 Tupac Shakur alimwambia msanii Madonna kwamba alivunja uhusiano wao wa kimapenzi kutokana na rangi ya ngozi yake katika barua iliojawa na hisia kwa msanii huyo wa muziki wa rap.

Barua hiyo ya 1995 ilioandikwa kwa ''M'' ilisema kuwa na mwanamume mweusi kungeweza kumsaidia kikazi lakini hatua hiyo itawaudhi mashabiki wake.

Madonna alithibitisha miaka miwili iliopita kwamba alikuwa na uhusiano na Tupac Shakur ijapokuwa haijulikani ulichukua muda gani.

Barua hiyo inapigwa mnada huku bei yake ya kwanza ikiwa $ 100,000, Ikiwa imeandikwa tarehe 15 mwezi Januari 1995, iliandikwa wakati Tupac alipokuwa akihudumia kifungo jela kwa unyanyasaji wa kingono na ilijiri miezi 18 kabla ya yeye kuuawa kwa kupigwa risasi.

Wasanii wote wawili walikuwa na umaarufu mkubwa na ''Kwa wewe kuonekana na mtu mweusi hakungedhuru kazi yako kivyovyote na badala yake kungefanya uonekana mtu uliye wazi na wa kufurahisha, Tupac aliyekuwa na umri wa miaka 23 alimwandikia Madonna akiwa katika Jela ya New York Clinton.

''Lakini kwangu mimi nilihisi kana kwamba kulingana na vile watu wanavyonichukulia ningewaudhi nusu ya watu walionifanya kuwa nilivyo',aliandika Madonna
''Kama ulivyosema, sijakuwa rafiki ambaye najua naweza kuwa'', aliandika Tupac , akiongezea, ''sikupenda kukuumiza moyo''.

Jarida la Rolling Stone lilithibitisha uhasilia wa barua hiyo ambayo ilichapishwa kwa mara ya kwanza na mtandao wa TMZ.

Tupac ambaye wazazi wake wote walikuwa wanaharakati wa Black Panther pia alisema kwamba Madonna wakati huo akiwa na umri wa miaka 36 alimuumiza moyo wakati aliposema katika mahojiano kwamba ''alikuwa amekwenda kuwabadili tabia wachezaji wote wa mpira wa kikapu pamoja na wasanii wote wa muziki wa rap''.

''Maneno hayo yaliniumiza moyo kwa sababu singedhani kwamba ulikuwa na uhisano mwengine na msanii yeyote wa rap isipokuwa mimi'', aliandika Tupac.

''Ni wakati huu ambapo baada ya kuumizwa moyo niliamua kujitetea na ndiposa nikasema mambo mengi''.

Aliongezea: tafadhali nielewe msimamo wangu wa awali kama kijana mdogo asiye na uzoefu.
Tupac alimalizia: Inafurahisha lakini uzoefu wangu umenifunza kutochukulia vitu vilivyo.

Mnamo mwezi Septemba tarehe 7 1996, msanii huyo ambaye aliuza rakodi milioni 75 duniani alifariki katika mfyatuliano wa risasi akiwa katika gari katika mji wa Las Vegas muda mfupi baada ya kutazama ndondi ambapo Mike Tyson alikuwa akizipiga.

Barua hiyo itapigwa mnada katika eneo la Gotta Have Rock and Roll Sale, ambao unatarajiwa kufanywa kati ya tarehe 18 na 19 mnamo mwezi Julai.

Ijumaa, 7 Julai 2017

Kwa mara ya kwanza Trump na Putin wamekutana Uso kwa Uso



Donald Trump na Vladimir Putin wamekutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza kabisa, na wakasalimiana kwa mikono huku mkutano wa G20 mjini Hamburg ukuanza.
Viongozi hao wa Marekani na Urusi wamesema wanataka kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambao uliathiriwa na tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.
Masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na biashara yanatarajiwa kutawala mazungumzo katika mkutano huo mkuu wa siku mbili.
Kumeshuhudiwa maandamano katika barabara nje ya eneo ambapo mkutano huo unafanyika.
Mke wa rais wa Marekani Melania Trump ameshindwa kuondoka katika hoteli ambapo amekuwa akikaa katika jiji hilo la Ujerumani kutokana na maandamano.
Alikuwa amepangiwa kufanya matembezi mafupi pamoja na wake wengine wa marais wanaohudhuria mkutano huo.
Lakini msemaji wake Stephanie Grisham amesema: "Polisi wa Hamburg walikataa kuturuhusu tuondoke."

Mbwana Samatta ametangaza kuwa balozi


 Nahodha wa timu ya taifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta leo kupitia ukurasa wake wa instagram ametangaza kuwa amekuwa balozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism).


Kupitia ukurasa wake wa instagrama Samatta aliandika “Nimefurahi kuwa balozi wa watu wenye ualbino tanzania.Nipo tayari kuwalinda na kushawishi watu wengine waendelee kuwalinda pia” >>> Samatta

 

mtoto wa Bradley Lowery amefariki leo



 Kama ni shabiki wa soka la England najua jina la Bradley Lowery sio geni katika masikio yako kutokana na umaarufu wa mtoto aliyekuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa kupenda sana kuishabikia Sunderland.

Bradley ambaye alikuwa ana mapenzi na Sunderland amefariki leo baada ya kusumbuliwa na kansa kwa muda mrefu, Bradley alikuwa akimpenda sana mshambuliaji wa zamani wa Sunderland ambaye amejiunga na AFC Bournemouth Jermain Defoe


 Shabiki huyo mtoto wa Sunderland aligundulika kuwa ana kansa akiwa na umri wa miezi 18 lakini amefariki leo akiwa na umri wa miaka 6, taarifa za kifo cha Bradley kimetolewa kupitia mitandao ya kijamii na wazazi wake.

Jumatano, 5 Julai 2017

Fahamu kuku wa maajabu aina ya ‘Ayam Cemani’ wenye nyama na mayai meusi.wanauzwa bei ya juu duniani

Tokeo la picha la ayam cemani

 Unaweza ukashangaa ila ndiyo hivyo kuwa Mungu ameumba viumbe wengi ambao pengine katika maisha yako viumbe wengine hutaweza kuwaona lakini sio kwa kuku aina ya Ayam Cemani ambao kila kitu kutoka kwenye miili yao ni cheusi kuanzia manyoya yao, Nyama na hadi mayai wanayototoa.

 Kuku hao ambao wanapatikana kwa wingi nchini Indonessia walianza kugundulika karne ya 17 kwenye visiwa vya Java na walikuwa wakitumika zaidi kwenye imani za kidini kwa kuwaabudu kuku hao.

Tokeo la picha la Ayam Cemani

Tokeo la picha la Ayam CemaniAsili ya jina la kuku hao linatokana na kijiji ambacho kuku hao walianza kupatikana karne 12 yaani Ayam maana yake ‘Chickens’ na Cameni ni kijiji kilichopo kwenye kisiwa cha Java huko Indonessia.


Kwa mujibu wa mfugaji na mtalaamu wa masuala ya ndege wanaoliwa Bw. Paul Bradshaw kutoka Marekani kwenye mahojiano yake na mtandao wa Greenfire Farm amesema mayai yake yana virutubisho mara mbili ya kuku wa kawaida na pia hata nyama yake ina utofauti kidogo na kuku wa kawaida.
Hata hivyo mtaalamu huyo amesema wateja wengi wanaulizia nyama yake wengi wao wakiamini kuwa ulaji wa nyama hiyo huongeza kinga ya mwili.
Ingawaje bado hakuna tafiti zozote za kibailojia kuhusu ukweli huo mpaka sasa lakini watu wengi wa Indonesia wanaamini ulaji wa mayai mabichi ya kuku hao huondoa sumu mwilini na ni tiba kwa akina mama wanaoshikwa na uchungu wa uzazi kwa muda mrefu.
Mpaka sasa ni utafiti mmoja tuu uliofanywa na Mwanasayansi,  Jan Steverink kutoka Uholanzi ambaye alibaini kuwa rangi nyeusi ya kuku hao inatokana na ongezeko la rangi kwenye tishu baada ya mabadiliko ya kijenetiki yajulikanayo kwa lugha ya kitaalamu kama (Fibromelanosis).
Kuku hao ambao wamejizolea umaarufu nchini Indonesia wamempa jina la gari la kifahari aina Lamborghini na hao wanamuita ‘Lamborghini of poultry’.
Kwa bei ya Marekani yai moja la kuku hao huuzwa mpaka dola $130 sawa na Tsh laki 2.9k, huku kuku mzima akiuzwa dola $2,500 sawa na Shilingi milioni 5.5 za kitanzania.


Tokeo la picha la Ayam Cemani chanzo na  mtandao ,bongo 5.

Taifa Stars washindwa kufurukuta mbele ya Zambia

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetupwa nje ya michuano ya COSAFA baada ya kipigo cha goli 4-2 kutoka kwa timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo.


Stars ilianza kupata bao kupitia Erasto Nyoni lakini Zambia wakasawazisha na kuongeza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1.
Baada ya Nyoni kuumia na kutolewa, mabeki wa kati Salim Mponde na Abdi Banda wakaonekana kuyumba na kutoa nafasi kwa Washambuliaji wa Zambia kuongeza mashambulizi
Kipindi cha pili, Zambia walipata mabao mawili ya haraka na kuwa 4-1 lakini Simon Msuva alifunga bao lingine la kufuta machozi na matokeo ya mpaka dakika ya 90 4-2.
Hata hivyo Taifa Stars kwa matokeo hayo itasubiri mshindi wa mechi ya baadae kati ya Lesotho na Zimbabwe na kucheza nae Ijumaa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo ya COSAFA.

Kilichoendelea baada ya Mahakama kuhamia Hospitali kumsomea mashtaka Manji




Leo July 5 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ililazimika kuhamia kwa muda  katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kumsomea mashtaka saba ya uhujumu uchumi, mfanyabiashara Maarufu Yusufu Manji na wenzake watatu. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Manji kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka kutokana na kulazwa katika taasisi hiyo.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, jopo la Mawakili Waandamizi wa serikali wakiongozwa na Mutalemwa Kishenyi, Nassoro Katuga na Tulumanywa Majigo.
Washtakiwa hao wanadaiwa walijipatia bidhaa isivyo halali mnamo Juni 30,2017 katika maeneo ya Chang’ombe A Temeke Jijini Dar es Salaam walikutwa na askari polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh milioni 192.5 ambazo zilipatikana isivyo halali.
Katika shitaka jingine inadaiwa washtakiwa hao walikutwa na mhuri wa serikali wa JWTZ isivyo halali Juni mnamo 30,2017 ambao umeandikwa” Mkuu wa Kikosi 121 kikosi cha JWTZ” bila ya kuwa na uhalali na kwamba kitendo hicho kinahatarisha uchumi na Usalama wa nchi.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu mashtaka hao Kwa sababu makosa hayo hapo chini ya uhujumu uchumi na Usalama wa taifa. Hata hivyo, upande wa mashtaka uliwasilisha hati ya pingamizi la dhamana kutokana Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma(DPP).
Katika hati hiyo, DPP alidai,ikiwa washtakiwa hao watapewa dhamana wanaweza kuhatarisha Usalama na maslahi ya nchi na Kwa mujibu wa sheria kulingana na shtaka la 1 na 2, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kisheria ya kutoa dhamana Kwa washtakiwa hao.
Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa na upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Hudson Ndusyepo alidai kuwa mashtaka hayo yanaiondolea mahakama kuwafikiria wateja wake dhamana.
Kutokana na kuwepo Kwa mabishani ya kisheria,Hakimu Shaidi alisema masuala yanapaswa kuongelewa kwenye mahakama yenye mamlaka kisheria Kwa sababu DPP hajaipa mamlaka ya kisheria ya mahakama ya Kisutu kusikiliza maombi ya dhamana. Kutokana na hali hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 19,mwaka huu Kwa ajili ya kutajwa

BREAKING: Ilipofikia kesi ya Mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent




Tunakumbuka ajali ya basi la Wanafunzi wa Lucky Vincent iliyotokea Karatu, Arusha na kuua 32 na kuacha Majeruhi watatu ambao wanatibiwa kwenye Hospitali ya Mercy, Sioux City Iowa, Marekani huku Mmiliki wa shule hiyo na Makamu Mkuu wa Shule wakishikiliwa na Polisi.
Sasa new story leo July 5, 2017 ni kwamba Mahakama ya Wilaya Arusha imesema kuwa Upelelezi wa kesi inayomkabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent, Innocent Mosha na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Longino Vincent umekamilika na kesi hiyo itaanza kusikilizwa July 26, 2017 wakikabiliwa na mashtaka matano.
Mashtaka wanayokabiliwa nayo pamoja na Mmiliki huyo kuruhusu Dereva kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, kutumia gari bila kuwa na BIMA pamoja na kushindwa kuingia mkataba na Mwajiriwa.
Mashtaka mengine ni kuzidisha abiria 13 kwenye gari pamoja Kaimu Mkuu wa Shule kuratibu safari na kuruhusu gari kuzidisha abiria.

Jumamosi, 1 Julai 2017

Manny Pacquiao kuzichapa na Jeff Horn kesho

anny Pacquiao (kushoto) akitunishiana msuli na Jeff Horn wakati wa kupima uzito jana Uwanja wa Suncorp kuelekea pambano lao la kesho kutetea ubingwa wake wa WBO uzito wa Welter mjini Brisbane nchini Australia

RIPOTI KAMILI: Sakata la mama aliyedai kuibiwa mtoto Hospitali ya Temeke




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa tume huru aliyoiunda ili kuchunguza malalamiko ya Asma Juma kuhusu kuibiwa mtoto mmoja kati ya mapacha wawili katika hospitali ya Rufaa ya Temeke Dar es salaam.
 Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa tume hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama Dkt. Charles Majige ambapo imeeleza kuwa Asma Juma hakuwa na watoto mapacha kama ilivyodaiwa na mlalamikaji huyo kutokana na kipimo cha Utra sound kukosea katika uchukuaji picha ya mtoto akiwa tumboni.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Charles Majige Amesema kuwa Asma aliamini hivyo kwa sababu Hospitali ya temeke hawakumchukua vipimo vya picha bali walitumia taarifa ya vipimo vya awali .
Aidha Dkt. Majige amesema kuwa tume hiyo imebaini kuwa Asma hakuibiwa mtoto na alikuwa hana mapacha kwa sababu uzito wake ulikua sio wa kubeba watoto wawili na katika chumba cha upasuaji kulikua na wataalamu 6 kutoka vitengo mbalimbali.