Producer wa muziki bongo Abydad amedai kudhulumiwa wimbo aliokuwa
amemuandalia msanii wake kisha kupatiwa msanii Ommy Dimpoz ambaye siku
ya jana ameuachia rasmi ulichukuliwa na mtayarishaji Lolli Pop
(GoodLuck Gozbert) kwa ajili ya kuuboresha.
Akizungumza leo kwenye kipindi cha Planet Bongo Abydad amesema kwamba
ameshtushwa sana kuusikia wimbo mpya wa Ommy Dimpoz kwani yeye na msanii
wake walikuwa katika hatua za mwisho za kufanya video baada ya Loly Pop
kuanza kumpiga kalenda kurudisha wimbo aliodai anaenda kuufanyia
maboresho.

Hii ni project yangu ambayo niliifanya
na msanii wangu mchanga anayeitwa Modala tangu Januari mwaka jana.
Wakati naiandaa Lolli Pop alikuwa studio na yeye alishauri kwamba
tumsaidie mdogo wetu atoke, kwa hiyo huu wimbo tuuboreshe vitu na kwa
vile sisi tuna tabia ya kushirikiana sikuona shida kumpatia kwa kuwa
nilimuamini sasa nilikuja kushtuka baada ya jana kuusikia Ommy
anautambulisha alafu anasema kaandikiwa na Lolli Pop" Abydad alifunguka.

Mwanamuziki na Mtayarishaji wa muziki Lolli Pop (Goodluck Gozbert)
Pamoja na hayo Abydad amesema kwamba hataweza kuchukua hatua zozote kwa
ajili ya kitendo hicho bali amewaaonya watu wote wenye tabia za aina
hiyo waweze kuziacha kwani kunaua vipaji vya vijana wenye ndoto za
kufikia mafanikio kama waliyonayo wa
chanzo na muungwana blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni