Stars ilianza kupata bao kupitia Erasto Nyoni lakini
Zambia wakasawazisha na kuongeza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa
mabao 2-1.
Baada ya Nyoni kuumia na kutolewa, mabeki wa kati Salim
Mponde na Abdi Banda wakaonekana kuyumba na kutoa nafasi kwa
Washambuliaji wa Zambia kuongeza mashambulizi
Kipindi cha pili, Zambia walipata mabao mawili ya haraka
na kuwa 4-1 lakini Simon Msuva alifunga bao lingine la kufuta machozi
na matokeo ya mpaka dakika ya 90 4-2.
Hata hivyo Taifa Stars kwa matokeo hayo itasubiri mshindi wa mechi
ya baadae kati ya Lesotho na Zimbabwe na kucheza nae Ijumaa kutafuta
mshindi wa tatu wa michuano hiyo ya COSAFA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni