Alhamisi, 31 Mei 2018

RATIBA YA SIMBA, YANGA KATIKA SPORTPESA SUPER CUP KULE KENYA IKO HIVI...






Ratiba ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018, inayotarajiwa kuanza kuunguruma Juni 3 mpaka 10, mwaka huu katika Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya, tayari imetoka ambapo Yanga itafungua mashindano hayo kwa kumenyana na Kakamega Homeboys ya Kenya.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 7:00 mchana, huku Gor Mahia ambayo nayo ni ya Kenya ikipambana na JKU ya Zanzibar kuanzia saa 9:15 alasiri. Mechi hizo zote zitachezwa Juni 3.

Simba ya Tanzania, wao watacheza siku inayofuata dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya mchezo utakaopigwa majira ya saa 9:00 alasiri ambapo siku hiyo itachezwa mechi hiyo pekee. Juni 5, AFC Leopards ya Kenya itakutana na Singida United kutoka Tanzania.
Mmoja wa waratibu wa michuano hiyo, Sabrina Msuya, alisema, maandalizi yote yako vizuri na timu kutoka Tanzania ambazo ni Simba, Yanga na JKU zinatarajiwa kuondoka kesho Alhamisi, huku Singida United ikisubiri mpaka imalize mechi yake ya Kombe la FA itakayochezwa Jumamosi hii.

“Mambo tayari yako safi kabisa kwani ratiba imetoka na timu za hapa nchini zitaondoka Alhamisi kuanzia saa 3:00 asubuhi ambapo Simba ndiyo itakuwa ya kwanza ikifuatiwa na JKU ambayo itaondoka Saa 7:00 mchana na baadaye saa 11:00 jioni, Yanga itafuatia.

“Singida United yenyewe itaondoka mara tu baada ya mchezo wake wa FA unaotarajiwa kufanyika Juni 2, mwaka huu huko Arusha,” alisema Sabrina.

Jumanne, 29 Mei 2018

Jezi mpya watakazotumia Real Madrid msimu wa 2018/2019






Club ya Real Madrid ikiwa zimepita siku nne toka watwae Kombe lao tatu mfululizo na 13 kwa jumla la UEFA Champions League, leo wameonesha rasmi jezi zao mpya watakazotumia msimu wa 2018/2019.

Real Madrid watatumia jezi mpya ambazo zitakuwa na tofauti ndogo na msimu ulioisha hizi zikiwa na michirizi mieusi na sio blue kama msimu uliyoisha lakini zimebadilishwa pia muonekano kwa kiasi flani.



uma Nature atoa ngoma mbili kwa mpigo, aponda uamuzi wa Q Chief

Msanii mkongwe wa muziki, Juma Nature baada ya ukimya wa miaka 3 ameachia nyimbo mbili kwa mpigo kwaajili ya kuwaburudisha mashabiki wake ambao walimmiss kwa miaka mingi.

‘Nadhani’ ni mmoja kati ya nyimbo hizo zilizoachiwa Jumanne na kusikilizwa kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm.

Akizungumza na kituo hicho cha redio, Nature alizungumzia ukimya wake namna alivyoipokea kauli ya Q Chief kuacha muziki.

“Mimi nilimsikiliza Q Chief mwanzo mwisho, alikuwa anazingua,” alisema Nature “Mtu ambaye anafanya muziki kwa miaka yake yote hawezi kuacha muziki kwa namna hiyo labda unaweza kukaa kimya kutokana na mambo fulani halafu baadae unarejea,”

Katika hatua nyingine mkongwe huyo alidai yupo tayari kujiunga na kundi lolote la muziki likiwemo kundi la TKM ambalo alifanya nalo kazi kipindi cha nyuma.

Pia alisema wasanii ambao angependa kuunda nao kundi ni Stamina kutoka Rostam pamoja na G.Nako kutoka kundi la Weusi

MAAJABU: Malapa yanayojiendesha kama gari

Kadri siku zinavyosonga ndivyo Wanasayansi wanavyoumiza kichwa ili kurahisisha utendaji wa baadhi ya mambo, leo May 29, 2018 nakusogezea hii ya kampuni ya Nissan Motor Co. ya nchini Japan imetengeza MALAPA yanayoitwa ‘ProPilot Park Ryokan’ ambayo  yanajiendesha.
Malapa hayo yana uwezo ya kujiweka sehemu wanapoingilia wageni ili wayatumie kisha kujirudisha tena sehemu ya kuingilia baada ya wageni kumaliza kuyatumia.
Malapa hayo yametengezwa na vihisio (sensor) vinavyowezesha kujiendesha kwenye sakafu ya mbao kwa kutumia teknolojia ya Nissan’s ProPilot Park.

Snoop Dogg ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia

Staa wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Calvin Cordozar Broadus ambaye wengi wanamfahamu kwa jina maarufu la Snoop Dogg amerudi tena kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia “Guinness World Record”, ambapo ili uweze kuingia katika kitabu hicho cha rekodi unatakiwa kufanya kitu ambacho cha kipekee.

Snoop Dogg mwenye umri wa miaka 46 amefanikiwa kuingia katika kitabu hicho kufuatia kufanikiwa kwa jaribio lake la kutengeneza cocktail yenye ujazo mkubwa zaidi duniani unaotajwa kufikia lita 500, baada ya kuchanganywa chupa 180 za Gin na chupa 154 Apricot pamoja na juisi ya machungwa.

Taarifa hizo za Snoop Dogg kufanikiwa kuingia kwenye kitabu cha rekodi ya dunia zinakuja zikiwa zimepita siku 74 toka atangaze rasmi kutoa album yake ya nyimbo za injili inayojulikana kwa jina la Bible of Love, maamuzi ambayo aliyafanya baada ya kutoa album 15 za muziki wa kidunia.

Ratiba ya Super Cup hii hapa, Yanga na Simba kukutana mapema

Simba na Yanga zinaweza kujikuta zinakutana mwaka huu kwa mara ya tatu mfulilizo lakini safari hii ikiwa ni katika michuano ya  SportPesa Super Cup.

Michuano hiyo inafanyika jijini Nairobi, Kenya na itakutanisha timu nane kutoka Tanzania na nne za wenyeji Kenya.

Michuano ya  SportPesa Super Cup inaanza Juni 3 hadi Juni 10 na Simba wataanza Sharks ya Kenya wakati Yanga baadaye watakuwa uwanjani dhidi ya Homeboyz.

Kama kila timu itashindana, uwezekano wa kukutana ni asilimia kubwa na kila mmoja atalazimija kujiweka vizuri mapema kabisa.

Huyu ndie Katibu Mkuu Mpya wa CCM Taifa

Leo May 29, 2018 Dkt. Bashiru Ali Kakurwa ndiye aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo alipendekezwa na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini DSM.
Hii ni baada ya Aliyekuwa Katibu Mkuu Kinana kuomba kujiuzulu na kukubaliwa na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.
Imethibitishwa katika taarifa ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) iliyoketi tarehe 28-29 May 2018 Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Bashiru Ally alikuwa Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na Rais Magufuli kufanya Uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi CCM.

Jumatatu, 28 Mei 2018

BUNGE LAOMBOLEZA

Image result for bunge la tanzania ndani

 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson leo asubuhi ameahirisha Bunge hadi kesho saa tatu asubuhi kupisha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, Mwl. Kasuku Bilago aliyefariki siku ya Jumamosi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa bungeni kesho Jumanne kuanzia saa 6 mchana na kuzikwa jimboni kwake keshokutwa, Jumatano.

KENYA WAANZA KAMATA KAMATA YA MAFISADI:

Image may contain: 3 people, people standing and outdoor


  Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa nchini Kenya (NYS) Richard Ndubai, pamoja na maafisa wengine wakuu, wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za ufisadi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma aliyeagiza kushtakiwa kwa washukiwa wote waliotajwa katika kashfa ya Shilingi bilioni tisa (9).
Maagizo ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma, Noordin Haji yametolewa baada ya kupokea taarifa kuhusu kampuni 10 na zaidi ya watu 40 binafsi waliotajwa katika sakata hiyo ya NYS Scandal kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Uhalifu, George Kinoti.
"Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka ya Umma amechunguza nyaraka zinazohusiana na sakata linaloendelea katika NYS na ameagiza mashtaka yafunguliwe mara moja dhidi ya wote waliotajwa kushukiwa ," iliandika ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatatu asubuhi.




Image may contain: 1 person, indoor

 Image may contain: 1 person, walking and outdoor

SALUTI KWA 'KING' JAMES

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Cleveland Cavaliers, LeBron James leo alfajiri amedhihirisha kuwa yeye ni 'Mfalme' wa kizazi cha sasa cha wachezaji wa kikapu baada ya 'kuibeba' timu yake na kutinga fainali ya NBA kwa kuichapa Boston Celtics kwa vikapu 87 kwa 79.
James pekee alifunga vikapu 35 na kucheza dakika zote 48 za mchezo huo.







Karius aomba msamaha Liverpool


KIPA wa Liv­erpool, Loris Karius, ame­waomba wenzake msamaha baada ya kufanya makosa kwenye  mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kipa huyo alifan­ya makosa ya ma­bao mawili kwenye mchezo huo, bao la kwanza lililofungwa na Karim Benzema na bao la tatu lilo­fungwa na Gareth Bale, na jana alitua England akiwa ameficha uso wake kwa aibu.

Liverpool kwenye mchezo huo ulio­pigwa Kiev nchini Ukraine, walichapwa 3-1 na malalamiko ya mashabiki wa timu hiyo yameangukia kwa kipa huyo raia wa Ujerumani, ambaye hata hivyo wache­zaji wenzake waliko­solewa kumtenga wal­ipomuacha peke yake akilia baada ya kipyenga cha mwisho, aka­onekana akifari­jiwa na wache­zaji wa Real Madrid tu.

“Nimeisaba­bisha timu yan­gu ikakosa ub­ingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, napen­da kumuom­ba msamaha kila mmoja kwenye timu ya Liverpool.



“Sijisikii vizuri leo, nimewaan­gusha wenzangu, na­jisikia vibaya sana, nafikiri makosa yangu ndiyo yamesababisha timu ipoteze ubingwa.

“Ni siku mbaya kwangu, lakini haya ndiyo maisha ya mak­ipa, unaweza kufanya makosa na lazima ua­mke na kupambana tena,” alisema Mjeru­mani huyo.



Liverpool walitua nchini England mape­ma jana asubuhi huku wachezaji wakiwa na huzuni.
LIVERPOOL, England

PICHA :Mapokezi ya Real Madrid baada ya kutua na taji la 13 la Champions League

Baada ya club ya Real Madrid kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa fainali ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2918, walifanikiwa kutwaa taji lao la 13 la UEFA Champions League.

Pamoja na kuwa Real Madrid walikuwa ndio Mabingwa wa tetezi wa taji hilo wamefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa club ya kwanza kuwahi kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo, huku staa wao Cristiano Ronaldo akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji hilo mara tano.



















Mtoto aokolewa na ‘Spiderman’ Paris

Leo May 28, 2018 ‘Spiderman’ amepongezwa baada ya kupanda sehemu ya mbele ya ghorofa mjini Paris kumuokoa mtoto aliekuwa kwenye uzio wa baraza ya ghorofa ya nne kwenye jengo refu.
Video ya Mamoudou Gassam maarufu kama ‘Spiderman’ akimuokoa mtoto huyo ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Alivuka kutoka kwenye baraza moja hadi nyingine kwa muda wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto huyo aliyekuwa amekwama na kumsalimisha.
Meya wa Paris Anne Hidalgo pia alisifu sana ushujaa wa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 22, na akasema alimpigia simu kumshukuru.