Msanii mkongwe wa muziki, Juma Nature baada ya ukimya wa miaka 3
ameachia nyimbo mbili kwa mpigo kwaajili ya kuwaburudisha mashabiki wake
ambao walimmiss kwa miaka mingi.
‘Nadhani’ ni mmoja kati ya nyimbo hizo zilizoachiwa Jumanne na
kusikilizwa kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm.
Akizungumza na kituo hicho cha redio, Nature alizungumzia ukimya wake namna alivyoipokea kauli ya Q Chief kuacha muziki.
“Mimi nilimsikiliza Q Chief mwanzo mwisho, alikuwa anazingua,” alisema
Nature “Mtu ambaye anafanya muziki kwa miaka yake yote hawezi kuacha
muziki kwa namna hiyo labda unaweza kukaa kimya kutokana na mambo fulani
halafu baadae unarejea,”
Katika hatua nyingine mkongwe huyo alidai yupo tayari kujiunga na kundi
lolote la muziki likiwemo kundi la TKM ambalo alifanya nalo kazi kipindi
cha nyuma.
Pia alisema wasanii ambao angependa kuunda nao kundi ni Stamina kutoka Rostam pamoja na G.Nako kutoka kundi la Weusi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni