MAAJABU: Malapa yanayojiendesha kama gari
Kadri siku zinavyosonga ndivyo Wanasayansi wanavyoumiza kichwa ili kurahisisha utendaji wa baadhi ya mambo, leo May 29, 2018 nakusogezea hii ya kampuni ya Nissan Motor Co. ya nchini Japan imetengeza MALAPA yanayoitwa ‘ProPilot Park Ryokan’ ambayo yanajiendesha.
Malapa hayo
yana uwezo ya kujiweka sehemu wanapoingilia wageni ili wayatumie kisha
kujirudisha tena sehemu ya kuingilia baada ya wageni kumaliza kuyatumia.
Malapa hayo yametengezwa na vihisio (sensor) vinavyowezesha kujiendesha kwenye sakafu ya mbao kwa kutumia teknolojia ya Nissan’s ProPilot Park.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni