Jumanne, 29 Mei 2018

Snoop Dogg ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia

Staa wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Calvin Cordozar Broadus ambaye wengi wanamfahamu kwa jina maarufu la Snoop Dogg amerudi tena kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia “Guinness World Record”, ambapo ili uweze kuingia katika kitabu hicho cha rekodi unatakiwa kufanya kitu ambacho cha kipekee.

Snoop Dogg mwenye umri wa miaka 46 amefanikiwa kuingia katika kitabu hicho kufuatia kufanikiwa kwa jaribio lake la kutengeneza cocktail yenye ujazo mkubwa zaidi duniani unaotajwa kufikia lita 500, baada ya kuchanganywa chupa 180 za Gin na chupa 154 Apricot pamoja na juisi ya machungwa.

Taarifa hizo za Snoop Dogg kufanikiwa kuingia kwenye kitabu cha rekodi ya dunia zinakuja zikiwa zimepita siku 74 toka atangaze rasmi kutoa album yake ya nyimbo za injili inayojulikana kwa jina la Bible of Love, maamuzi ambayo aliyafanya baada ya kutoa album 15 za muziki wa kidunia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni