Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa nchini Kenya (NYS) Richard Ndubai, pamoja na maafisa wengine wakuu, wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za ufisadi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma aliyeagiza kushtakiwa kwa washukiwa wote waliotajwa katika kashfa ya Shilingi bilioni tisa (9).
Maagizo ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma, Noordin Haji yametolewa baada ya kupokea taarifa kuhusu kampuni 10 na zaidi ya watu 40 binafsi waliotajwa katika sakata hiyo ya NYS Scandal kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Uhalifu, George Kinoti.
"Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka ya Umma amechunguza nyaraka zinazohusiana
na sakata linaloendelea katika NYS na ameagiza mashtaka yafunguliwe mara
moja dhidi ya wote waliotajwa kushukiwa ," iliandika ofisi ya mwendesha
mashtaka wa umma kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatatu asubuhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni