mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania
blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla
kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Club ya Real Madrid ikiwa zimepita siku nne toka watwae Kombe lao tatu mfululizo na 13 kwa jumla la UEFA Champions League, leo wameonesha rasmi jezi zao mpya watakazotumia msimu wa 2018/2019. Real Madrid watatumia jezi mpya ambazo zitakuwa na
tofauti ndogo na msimu ulioisha hizi zikiwa na michirizi mieusi na sio
blue kama msimu uliyoisha lakini zimebadilishwa pia muonekano kwa kiasi
flani.
Msanii mkongwe wa muziki, Juma Nature baada ya ukimya wa miaka 3
ameachia nyimbo mbili kwa mpigo kwaajili ya kuwaburudisha mashabiki wake
ambao walimmiss kwa miaka mingi.
‘Nadhani’ ni mmoja kati ya nyimbo hizo zilizoachiwa Jumanne na
kusikilizwa kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm.
Akizungumza na kituo hicho cha redio, Nature alizungumzia ukimya wake namna alivyoipokea kauli ya Q Chief kuacha muziki.
“Mimi nilimsikiliza Q Chief mwanzo mwisho, alikuwa anazingua,” alisema
Nature “Mtu ambaye anafanya muziki kwa miaka yake yote hawezi kuacha
muziki kwa namna hiyo labda unaweza kukaa kimya kutokana na mambo fulani
halafu baadae unarejea,”
Katika hatua nyingine mkongwe huyo alidai yupo tayari kujiunga na kundi
lolote la muziki likiwemo kundi la TKM ambalo alifanya nalo kazi kipindi
cha nyuma.
Pia alisema wasanii ambao angependa kuunda nao kundi ni Stamina kutoka Rostam pamoja na G.Nako kutoka kundi la Weusi
Kadri siku zinavyosonga ndivyo Wanasayansi wanavyoumiza kichwa ili kurahisisha utendaji wa baadhi ya mambo, leo May 29, 2018 nakusogezea hii ya kampuni ya Nissan Motor Co. ya nchini Japan imetengeza MALAPA yanayoitwa ‘ProPilot Park Ryokan’ ambayo yanajiendesha. Malapa hayo
yana uwezo ya kujiweka sehemu wanapoingilia wageni ili wayatumie kisha
kujirudisha tena sehemu ya kuingilia baada ya wageni kumaliza kuyatumia. Malapahayo yametengezwa na vihisio (sensor) vinavyowezesha kujiendesha kwenye sakafu ya mbao kwa kutumia teknolojia ya Nissan’s ProPilot Park.
Staa wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Calvin Cordozar Broadus ambaye wengi wanamfahamu kwa jina maarufu la Snoop Dogg amerudi tena kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia “Guinness World Record”, ambapo ili uweze kuingia katika kitabu hicho cha rekodi unatakiwa kufanya kitu ambacho cha kipekee. Snoop Dogg
mwenye umri wa miaka 46 amefanikiwa kuingia katika kitabu hicho kufuatia
kufanikiwa kwa jaribio lake la kutengeneza cocktail yenye ujazo mkubwa
zaidi duniani unaotajwa kufikia lita 500, baada ya kuchanganywa chupa
180 za Gin na chupa 154 Apricot pamoja na juisi ya machungwa.
Taarifa hizo za Snoop Dogg
kufanikiwa kuingia kwenye kitabu cha rekodi ya dunia zinakuja zikiwa
zimepita siku 74 toka atangaze rasmi kutoa album yake ya nyimbo za
injili inayojulikana kwa jina la Bible of Love, maamuzi ambayo aliyafanya baada ya kutoa album 15 za muziki wa kidunia.
Simba na Yanga zinaweza kujikuta zinakutana mwaka huu kwa mara ya tatu
mfulilizo lakini safari hii ikiwa ni katika michuano ya SportPesa Super
Cup.
Michuano hiyo inafanyika jijini Nairobi, Kenya na itakutanisha timu nane kutoka Tanzania na nne za wenyeji Kenya.
Michuano ya SportPesa Super Cup inaanza Juni 3 hadi Juni 10 na Simba
wataanza Sharks ya Kenya wakati Yanga baadaye watakuwa uwanjani dhidi ya
Homeboyz.
Kama kila timu itashindana, uwezekano wa kukutana ni asilimia kubwa na kila mmoja atalazimija kujiweka vizuri mapema kabisa.
Leo May 29, 2018 Dkt. Bashiru Ali
Kakurwa ndiye aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ambapo alipendekezwa na kupitishwa na wajumbe wote
waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini DSM. Hii ni baada ya Aliyekuwa Katibu Mkuu
Kinana kuomba kujiuzulu na kukubaliwa na Rais Magufuli ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa. Imethibitishwa katika taarifa ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) iliyoketi tarehe 28-29 May 2018 Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Bashiru Ally alikuwa Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na Rais Magufuli kufanya Uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi CCM.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson leo asubuhi ameahirisha Bunge
hadi kesho saa tatu asubuhi kupisha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa
Mbunge wa Buyungu, Mwl. Kasuku Bilago aliyefariki siku ya Jumamosi
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa bungeni kesho Jumanne kuanzia saa 6 mchana na kuzikwa jimboni kwake keshokutwa, Jumatano.
Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa nchini Kenya (NYS)
Richard Ndubai, pamoja na maafisa wengine wakuu, wamekamatwa na polisi
kwa tuhuma za ufisadi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma aliyeagiza kushtakiwa kwa washukiwa wote
waliotajwa katika kashfa ya Shilingi bilioni tisa (9).
Maagizo ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma, Noordin Haji yametolewa baada ya kupokea taarifa kuhusu kampuni 10 na zaidi ya watu 40 binafsi waliotajwa katika sakata hiyo ya NYS Scandal kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Uhalifu, George Kinoti.
"Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka ya Umma amechunguza nyaraka zinazohusiana
na sakata linaloendelea katika NYS na ameagiza mashtaka yafunguliwe mara
moja dhidi ya wote waliotajwa kushukiwa ," iliandika ofisi ya mwendesha
mashtaka wa umma kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatatu asubuhi.
Mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Cleveland Cavaliers, LeBron
James leo alfajiri amedhihirisha kuwa yeye ni 'Mfalme' wa kizazi cha
sasa cha wachezaji wa kikapu baada ya 'kuibeba' timu yake na kutinga
fainali ya NBA kwa kuichapa Boston Celtics kwa vikapu 87 kwa 79.
James pekee alifunga vikapu 35 na kucheza dakika zote 48 za mchezo huo.
KIPA wa Liverpool, Loris Karius, amewaomba wenzake msamaha baada ya
kufanya makosa kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kipa huyo alifanya makosa ya mabao mawili kwenye mchezo huo, bao la
kwanza lililofungwa na Karim Benzema na bao la tatu lilofungwa na
Gareth Bale, na jana alitua England akiwa ameficha uso wake kwa aibu.
Liverpool kwenye mchezo huo uliopigwa Kiev nchini Ukraine, walichapwa
3-1 na malalamiko ya mashabiki wa timu hiyo yameangukia kwa kipa huyo
raia wa Ujerumani, ambaye hata hivyo wachezaji wenzake walikosolewa
kumtenga walipomuacha peke yake akilia baada ya kipyenga cha mwisho,
akaonekana akifarijiwa na wachezaji wa Real Madrid tu.
“Nimeisababisha timu yangu ikakosa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya,
napenda kumuomba msamaha kila mmoja kwenye timu ya Liverpool.
“Sijisikii vizuri leo, nimewaangusha wenzangu, najisikia vibaya sana,
nafikiri makosa yangu ndiyo yamesababisha timu ipoteze ubingwa.
“Ni siku mbaya kwangu, lakini haya ndiyo maisha ya makipa, unaweza
kufanya makosa na lazima uamke na kupambana tena,” alisema Mjerumani
huyo.
Liverpool walitua nchini England mapema jana asubuhi huku wachezaji wakiwa na huzuni.
LIVERPOOL, England
Baada ya club ya Real Madrid kufanikiwa kupata ushindi wa
magoli 3-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa fainali ya UEFA Champions
League msimu wa 2017/2918, walifanikiwa kutwaa taji lao la 13 la UEFA
Champions League.
Pamoja na kuwa Real Madrid walikuwa ndio Mabingwa wa tetezi wa taji
hilo wamefanikiwa kuweka rekodi ya kuwa club ya kwanza kuwahi kutwaa
taji hilo mara tatu mfululizo, huku staa wao Cristiano Ronaldo akiweka
rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji hilo mara tano.
Leo May 28, 2018
‘Spiderman’ amepongezwa baada ya kupanda sehemu ya mbele ya ghorofa
mjini Paris kumuokoa mtoto aliekuwa kwenye uzio wa baraza ya ghorofa ya
nne kwenye jengo refu. Video ya Mamoudou Gassam maarufu kama ‘Spiderman’ akimuokoa mtoto huyo ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Alivuka kutoka kwenye baraza moja hadi
nyingine kwa muda wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto huyo aliyekuwa
amekwama na kumsalimisha. Meya wa Paris Anne Hidalgo pia alisifu
sana ushujaa wa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 22, na akasema
alimpigia simu kumshukuru.