Jumanne, 25 Julai 2017

Ma-RC Ma-DC Watakao lia Njaa watangaziwa kiama



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amewambia Wakuu wa Mikoa na Wilaya watakao  Dhihirisha Mikoa/wilaya zao kuwa zina njaa hawafai kuwa Mkuu wa Mkoa wilaya hiyo

hayo yameelezwa leo na Rais Magufuli alipokuwa Ziarani Mkaoni Sindida ambapo ameeleza kuwa Serikali haitatoa Chakula kwa Wilaya au Mkoa utakao kuwa na Njaa na kwamba Ma-DC na ma-RC, wa sehemu husika hawatafaa kuwa kwenye nafasi hizo

 Rais Magufuli ameeleza kuwa Ma-Dc na Ma-RC wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha kazi kwa wananchi

TCU yasitisha udahili kwa vyuo 19 nchini



 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa imefanya uhakiki wa vyuo vyote vya elimu ya juu nchini ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni hapo, ripoti ya uhakiki huo ilionyesha mapungufu kadhaa katika baadhi vyuo.

Hivyo tume imeamua kuchukua uamuzi wa kusitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo hivyo.

Aidha, Tume hiyo imevitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na:
    1. Eckenforde Tanga University
    2. Jomo Kenyatta University, Arusha
    3. Kenyatta University, Arusha
    4. United African University of Tanzania
    5. International Medical and Technological University (IMTU)
    6. University of Bagamoyo
    7. Francis University College of Health and Allied Sciences
    8. Archibishop James University College
    9. Archibishop Mihayo University College
    10. Cardinal Rugambwa Memorial University College
    11. Kampala International University Dsm College
    12. Marian University College
    13. Johns University of Tanzania Msalato Centre
    14. Johns University of Tanzania, Marks Centre
    15. Joseph University College of Engineering and Technology
    16. Teofilo Kisanji University
    17. Teofilo Kisanji University Tabora Centre
    18. Tumaini University, Mbeya Centre
    19. Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo)

Aidha, kutokana na mapungufu hayo katika vyuo mbalimbali imeamriwa kuwa jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini zimesitishwa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18.

UTAFITI: Jaribio la kinga ya HIV kwa wanawake lafanikiwa



 Watafiti nchini Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia mpira wa mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa.


Utafiti zaidi sasa utafanyiwa vijana barani Afrika.
Wasichana walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na ukimwi , ambao hulibadilishwa kila mwezi baada ya kipindi cha miezi sita.
Ni mojawapo ya mipango ya kutengeza kifaa ambacho wanawake watatumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV ili wasiweze kuwategemea wanaume kuvaa mipira ya kondomu.
Wakiripoti ugunduzi huo mpya kuhusu virusi vya HIV mjini Paris, watafiti walisema kuwa wanafurahi kwamba wasichana hao walitumia mvirongo huo na kusema kuwa wameupenda.
Wanawake na wasichana walio na kati ya umri wa miaka 15-24 wanadaiwa kuwa moja kwa tano ya visa vyote vya maambukizi ya HIV duniani.
Takriban wanawake 1000 huambukizwa virusi kila siku katika Afrika ya jangwa la sahara.

Kijana Mdogo wa Kiafrika aushanga Ulimwengu kwa Kugundua Sachi Injini inayoitishia google



 Kijana wa Chuo Kikuu cha Ghana Gabriel Opare mwenye Umri wa Miaka 19 uashangaza ulimwengu kwa kugundua Sachi injini ambayo inauwezo unaofafania na Google.

Kijana huyo mdogo Raia wa Ghana ambaye anasomea Shahada ya Pili ya Sosholojia  kwenye chuo hicho amegundua Searchi Ingene hiyo yenye jina la 'Mudclo'

Yanga yamsajili golikipa wa Serengeti Boys



 Klabu ya Yanga yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es salaam, imefanikiwa kunasa saini ya Golikipa wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Ramadhani Kabwili.


Yanga SC wametoa taarifa hizo kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii kuwa amesaini kwa kandarasi ya miaka mitano.
“Ramadhani Kabwili,golikipa wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania (Serengeti Boys) amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka mitano”,imesomeka ripoti iliyotolewa na Yanga.
Klabu ya Yanga ni miongoni mwa klabu zilizosajili wachezaji wengi msimu hii ni kutokana na nguvu ya pesa walizopata baada ya udhamini wa Kampuni ya kubashiri ya SportPesa.

Jumamosi, 22 Julai 2017

Magoli ya Mbwana Samatta na Wayne Rooney timu zao zilipokutana leo



 
Jumamosi ya July 22 2017 mtanzania Mbwana Samatta alipata nafasi ya kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton FC inayodhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.




Mchezo wa Everton dhidi ya KRC Genk uliyochezwa nchini Ubelgiji katika uwanja wa Luminus Arena, umempa nafasi nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta kuonesha uwezo wake dhidi ya Everton ambayo ni miongoni mwa vilabu saba England ambavyo havijawahi kushuka daraja toka kuanzishwa kwa mfumo wa Ligi Kuu England 1992.


Mbwana Samatta ambaye ndio mshambuliaji tegemeo wa KRC Genk baada ya kuumia kwa mgiriki Nikolaos Karelis aliifungia KRC Genk goli la kusawazisha dakika ya 55, hiyo ni baada ya Wayne Rooney kuifungia Everton goli la kwanza dakika ya 45 kwa kutumia vyema assist ya Sandro Ramirez.



Rais Magufuli Atishia Kuifunga Migodi ya Madini Endapo Barrick Watachelewa Katika Mazungumzo




Wakati Kampuni ya Acacia ikisema imepoteza mapato ya Sh385 bilioni katika kipindi cha miezi sita kutokana na kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini nje, Rais John Magufuli ametishia kufunga migodi ya wawekezaji iwapo hawatajitokeza mapema katika mazungumzo.

Rais Magufuli amesema hayo takriban wiki moja baada ya kudokeza kuwa Serikali ingeanza mazungumzo “na waliokuwa wanatuibia” mapema wiki hii.

Jana, Rais Magufuli alisema Serikali haitasita kufunga migodi yote ya madini ambayo wamiliki walitakiwa kufanya mazungumzo na Serikali kuhusu ulipaji kodi.

 Akizungumza katika ziara yake mkoani Kigoma ambako alizindua Barabara ya Kibondo-Nyakanazi, Rais Magufuli alisema Taifa linapoteza fedha nyingi kutokana na upotevu wa madini.

“Ni matrilioni ya fedha ambayo yanapotea, na sasa hivi tumewaita tufanye mazungumzo lakini wakichelewachelewa nitafunga migodi yote,” alisema.

Alisema ni bora migodi hiyo ikakabidhiwa kwa Watanzania kuliko wawekezaji ambao hawalipi kodi.

Rais Magafuli alipiga marufuku usafirishaji wa mchanga huo nje ya nchi, na baadaye kuunda kamati mbili; moja ya kuchunguza kiwango cha madini kilichokuwa katika makontena 277 yaliyozuiwa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine kuangalia athari za kiuchumi na kisheria tangu mchanga huo uanze kusafirishwa mwaka 1998.

Ripoti ya kamati ya kwanza ilisema kuwa Acacia, inayoendesha migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, haikusema ukweli kuhusu kiwango cha dhahabu, ikidai kuwa imebaini mchanga huo una madini hayo mara kumi ya kiwango kilichotangazwa na wawekezaji hao.

Ripoti ya kamati ya pili ilionyesha kuwa katika kipindi cha miaka 20, Serikali ilipoteza zaidi ya Sh108 trilioni na kwamba Acacia haijasajiliwa nchini na hivyo inafanya kazi kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Acacia haijakubaliana na matokeo ya ripoti hizo, ikisema inataka uchunguzi wa kamati huru na kwamba kama matokeo hayo ni ya kweli, Tanzania ingekuwa moja ya nchi tatu zinazozalisha dhahabu kwa wingi duniani.

Jana, Acacia ilisema imepoteza Sh385 bilioni katika kipindi cha miezi sita. Acacia pia imesema endapo hali itaendelea kuwa hivyo, italazimika kuufunga mgodi wake wa Bulyanhulu na kusitisha mikataba ya ajira kwa wafanyakazi.

Hata hivyo, katika taarifa yake ya jana inayozungumzia kipindi cha Januari mpaka Juni, Acacia imesema  imepata changamoto kubwa katika utendaji wake nchini.

 “Nusu (ya kwanza), imetupa changamoto kubwa katika shughuli zetu Tanzania baada ya kuwekewa zuio la usafirishaji wa makinikia kuanzia Machi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia, Brad Gordon. “Mapato yetu yameshuka mpaka dola 175 milioni za Kimarekani kutoka dola 318 milioni tulizotarajia.”

Licha ya kushindwa kuingiza Dola 175 milioni za Marekani (zaidi ya Sh385 bilioni) zilizotarajiwa, Acacia inasema imelipa dola51 milioni za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambazo ni zaidi ya Sh112.2 bilioni.

Ili kulinda masilahi ya wanahisa wake, Acacia imewasilisha notisi kwa msuluhishi kwa ajili ya migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi ambayo ndiyo inayozalisha mchanga wa madini kwa sasa.

Buzwagi imekuwa ikisafirisha mchanga huo kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuuyeyusha ili kupata mabaki ya dhahabu, shaba na fedha kutokana na teknolojia hiyo kutokuwapo mgodini.

Hatua ya kwanza ya kuchenjua dhahabu hufanyika mgodini na mchanga unaosalia ndio unaosafirishwa nje. Acacia imekuwa ikieleza kuwa mchanga huo una asilimia 0.02 ya dhahabu wakati shaba ni asilimia 10.

Acacia pia imekanusha taarifa ya kuwapo amri ya kutakiwa kuondoka nchini kwa mmoja wa wafanyakazi wake wa kigeni.

“Hatuna taarifa za kutolewa kwa amri hiyo kwa mfanyakazi wetu yeyote wa kigeni aliyepo Tanzania. Tunashirikiana vizuri na Serikali kwenye mazungumzo yanayoendelea na hakuna aliyekamatwa habari hiyo si sahihi,” inasema taarifa hiyo.

Tandika: Daladala yagonga treni, wawili wafariki dunia




 Watu wawili wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea leo asubuhi ikihusisha gari ya abiria aina ya coaster kukigonga kichwa cha treni maeneo ya Yombo Devis Kona.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto amesema watu wawili wamefariki dunia akiwamo mwanamke mmoja na mwanaume mmoja ambaye ni kondakta wa daladala hiyo.
Muroto amesema mbali na watu wawili kufariki pia kuna majeruhi 36 wanne kati yao wakiwa mahututi.
Amesema majeruhi mahututi ni wanawake watatu na mwanaume mmoja.
“Majeruhi wite wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke na miongoni mwa majeruhi hao wanne wapo katika hali mbaya”amesema Kamanda Muroto.

Mfanyabiashara wa Madini Kilimanjaro aliyehukumiwa maisha jela



 Moja ya habari ambayo imekuwa gumzo ni hii inayotokea Kilimanjaro ambako Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha maisha jela mfanyabiashara wa Madini Benedict Kimario kwa makosa mawili ya ubakaji na ulawiti.

Ijumaa, 21 Julai 2017

Tundu Lissu agoma Kupimwa mkojo





 Tundu Lissu(Mb) amekataa kupimwa mkojo baada ya kufikishwa kwa Mkemia  
Asema kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi

Taarifa za awali ziliarifu kuwa, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa Kituo cha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.

Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

Agosti 8 ni Yanga Vs Singida United




Ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara, Yanga itaivaa Singida United katika mechi ya kirafiki itakayopigwa Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Tayari uongozi wa Singida United umethibitisha kuwepo kwa mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.
Timu zote mbili zinadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.


UPDATE: Polisi wameondoka na Tundu Lissu kituoni




Jana jioni Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge kutokea mkoa wa Singida Tundu Lissu alikamatwa na Polisi uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa anaelekea Rwanda ambapo alichukuliwa na kuendelea kushikiliwa na Polisi hadi leo.
Taarifa ambayo imetolewa mchana huu na Afisa habari wa CHADEMA ni kwamba Polisi wamemchukua  Tundu Lissu kutoka kituo kikuu cha polisi na wanaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kupekuliwa ambapo taarifa hiyo ya CHADEMA imesema hadi muda inapotolewa taarifa hii haujajulikana upekuzi huo unahusu kitu gani.
chanzo milrad blog .

Nitawanyoosha Yanga kulinda heshima yangu- Kichuya

Tokeo la picha la kichuya

 Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya ametamba kuendeleza ubabe dhidi ya Yanga kwa kutupia magoli kama msimu uliopita ili kulinda heshima yake.


Kichuya amesema hayo baada ya mashabiki wengi wa Klabu ya Yanga kuonekana wenye hofu naye hususani katika mchezo unaokuja wa ngao ya jamii utakaochezwa katika dimba la uwanja wa taifa.
Sipendi kuwa mwongeaji sana, ila napenda kufanya sana kazi uwanjani, naendelea kujipanga na naahidi kulinda heshima yangu, hata kama sitafunga lakini lazima nitoe pasi ya bao ili kuibeba Simba timu inayonifanya niishi mjini,” amesema Kichuya kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwanaspoti.
Kichuya ambaye yupo nchini Rwanda na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kufuzu michuano ya CHAN, alifunga bao la kusawazisha katika mechi iliyojaa utata ya Oktoba Mosi, 2016 dhidi ya Simba, kabla ya kufunga bao la ushindi mechi ya marudiano na kuwazima kabisa Yanga kwenye mechi zote mbili za msimu uliopita.
Simba na Yanga zitavaana Agosti 23 mwaka huu kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa uwanja wa Taifa, jijini Dare se salaam.