Jumatano, 31 Januari 2018

TAMISEMI yaagiza Shule ya Sekondari Njombe kuchunguzwa baada ya wanafunzi wote kupata 0






Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi, Joseph Kakunda ameagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Njombe kufanya uchunguzi wa matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Viziwi Njombe.


Katika matokeo yaliyotangazwa jana Jumanne Januari 30,2018 na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), shule hiyo katika matokeo ya mtihani uliofanyika Oktoba na Novemba mwaka jana watahiniwa wote 21 wamepata daraja sifuri (0).

Naibu Waziri Kakunda ametoa agizo la kufanyika uchunguzi leo Jumatano Januari 31,2018 bungeni alipojibu swali la mbunge wa Buyungu (Chadema), Samson Bilago.

Bilago alitaka kujua ni kwa nini shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu zinafanya vibaya kwenye mitihani.

Akizungumzia hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema walimu waliosoma elimu maalumu watapata ajira bila kikwazo cha kusubiri.

Mkuchika amesema wanasubiri kupelekewa orodha ya walimu hao.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini aliyetoa mfano wa shule ya Viziwi Njombe ya wanafunzi wa mahitaji maalumu iliyofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne akisema ni kutokana na kukosa walimu hao.

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari: Dk. Kigwangalla Aeleza Hatma Ya Wavamizi Katika Hifadhi Ya Bonde La Mto Kilombero

Mzee Majuto baada ya kutembelewa hospitalini na Rais Magufuli


Jumatano ya January 31 2018 Rais John Pombe Magufuli alimtembelea hospitalini muigizaji mzee Majuto, ambaye amelazwa hospitali ya Tumaini Upanga jijini Dar es Salaam, lengo likiwa kumjulia hali, Mzee Majuto anasumbuliwa na tatizo la tezi dume.

Maamuzi ya serikali ya Kenya kwa vituo vya TV vilivyoonesha ‘kuapishwa’ kwa Odinga

Waziri wa Mambo ya Ndani Kenya Fred Matiang’i amesema kuwa vyombo vitatu vya habari ambavyo vilifungwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo jana baada ya kurusha matangazo ya ‘kuapishwa’ kwa Kiongozi wa Upinzani NASA Raila Odinga, vitaendelea kufungwa.
Ameeleza kuwa vyombo hivyo ambavyo ni Citizen TV, KTN na NTV vitaendelea kuwa vimefungwa mpaka uchunguzi utakapofanyika kuhusiana na kile alichokiita ‘uvunjwaji wa usalama uliopindukia’ na kuwa umekamilika.
“Serikali ilifahamu na bado inafahamu jukumu la vyombo hivyo vya habari vilivyoshiriki katika uendelezaji wa jambo lililo kinyume na sheria. ushiriki wao ungeweza kusababisha vifo vya maelfu ya Wakenya wasio na hatia” – Fred Matiang’i

Ilipofikia kesi ya Mbunge Lijualikali na Suzan Kiwanga Mahakamani leo

Wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Morogoro, Peter Lijualikali na Susan Kiwanga pamoja na wafuasi wa chama hicho wapatao 55 wamefika katika Mahakama ya Hakimu mkazi wa mkoa huo kwa ajili ya kesi ya jinai namba 296 ya mwaka 2017 inayowakabili.
Wabunge hao pamoja na wafuasi wao wanatuhumiwa kwa makosa nane ikiwemo ya kuanzisha vurugu na kuchoma mali za umma katika Kata ya Sofi wilayani Malinyi wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani Novemba 26, mwaka jana ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 27 mwaka huu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mawikili wa utetezi wamesema, walikubaliana kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya mwezi kwa mujibu wa sheria licha ya kwamba haitaweza kusikilizwa kutokana na Mahakama Kuu kuhamia katika mahakama hiyo kwaajili ya kusikiliza kesi zinazowahusu.
Amesema, waliomba tarehe hiyo kwa lengo la kutajwa tu ili siku hiyo wapange tarehe ya kuanza kusikilizwa kwaajili ya kuwawezesha wateja wao waweze kumaliza kesi hiyo na kurejea katika majukumu yao. Wameiomba mahakama hiyo kutenda haki kwa kusikiliza kesi hiyo kwa haki ili kuondoa dhana iliyopo ya kwamba kesi hiyo inaendeshwa kisiasa

Aubameyang katua Arsenal Giroud kaondoka nae



kadhaa wa baada ya club ya Arsenal kuthibitisha kumsajili staa wa soka wa kimataifa wa Gabon aliyekuwa anaichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani Pierre-Emerick Aubameyang, mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa Arsenal Oliver Giroud ameondoka nae.

Giroud ameondoka Arsenal na kwenda kujiunga na club ya Chelsea kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 18 lakini Chelsea nao wamemtoa kwa mkopo mchezaji Batshuayi kwenda Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Oliver Giroud ameondoka Arsenal na kujiunga na Chelsea baada ya kudumu ndani ya club ya Arsenal kwa miaka sita alipojiunga nayo 2012 akitokea Montpellier.

MAGAZETI YA LEO 31/1/2018























Hii ndio gharama ya passport za kielektroniki



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.  Mwigulu Nchemba amesema kuwa gharama mpya ya hati ya kusafiria ya kielektroniki itakuwa Sh. 150,000.

Dk Nchemba amesema hayo leo  wakati wa uzinduzi wa Hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam ambapo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha Dkt. Miwgulu Nchemba amesema kuwa Pasipoti hizo zitakuwa na ukurasa zaidi ya mmoja  na mwonekano mpya.

“kiasi cha gharama hiyo  ni sawa na Sh15,000 kwa mwaka kwa sababu itatumika kwa miaka 10. Gharama za kupata pasipoti sasa ni TSh.50,000 na hutumika kwa miaka 10 tangu zilipotolewa,“ amesema Dkt. Mwigulu.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa gharama ya laki moja na nusu bei hiyo ni ya juu kidogo kuliko bei ya sasa . huku kieleza kuwa bei hiyo imezingatia ubora wa utenngenezaji wa Pasipoti hiyo.

Rais Magufuli amwaga Bilioni 10 idara ya Uhamiaji



 John Magufuli leo January 31, 2018 ametangaza kutoa Tsh Bilioni 10 kwa Idara ya Uhamiaji ambayo iko chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ili ijenge Makao Makuu yake Mjini Dodoma.
Rais Magufuli ametangaza kutoa pesa hiyo katika tukio la uzinduzi wa hati ya kusafiria ya kielektroniki Dar es Salaam na kueleza kuwa amefanya hivyo kama shukrani yake kwa Idara hiyo kwa jinsi ya utendaji wake siku za hivi karibuni.
“Dr. Makakala katafute eneo, nitawapa Tshs Bilioni 10, wakati wowote mtakapozihitaji muanze kujenga Makao Makuu ya Uhamiaji, na ninatoa hizi kama shukrani kwa kazi kubwa unayofanya wewe na watendaji wako.” – Rais John Magufuli.

Jumapili, 28 Januari 2018

#VPL Msimamo wa VPL baada ya mechi za leo: Simba 4 Majimaji 0 Singida United 1 Tanzania Prisons 0

No automatic alt text available.

#VPL Simba wanapata bao la 3 kupitia kwa kinara wao wa mabao, Emmanuel Okwi.

No automatic alt text available.

chadema wapata pigo tena jimbo la siha



Viongozi wote wa CHADEMA Kata ya Ormelili Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro wanadaiwa kujiuzulu nafasi zao kwenye chama hicho nakuomba kujiunga na CCM.
Viongozi hao wamepokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Polepole wakati wa Kampeni za kumnadi mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM , Jimbo la Siha Dk. Godwin Mollel.
Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na aliyekuwa amejitolea nyumba yake kutumika kama Ofisi ya CHADEMA, Kata ya Ormelili, Janneth Mamboleo Mushi ambao kwa pamoja wameomba kujiunga na CCM na kuchukua nyumba yake.



#VPL Nahodha John Bocco anaiandikia Simba bao la pili kwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Said Ndemla ikiwa ni dakika 10 tu baada ya kufunga bao la kwanza.

No automatic alt text available.

#VPL Simba wanapata bao la kuongoza kupitia kwa nahodha wao, John Bocco anayetumbukiza mpira wavuni kwa kichwa.

No automatic alt text available.

SASA NI MAUAJI YA KIMBARI DHIDI YA JAMII YA WATUTSI:



Umoja wa Mataifa (UN) umepitisha kwa kauli moja uamuzi wa kubadili jina la mauaji ya Rwanda kwa kupewa jina la 'mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya watutsi'.
Awali mauaji hayo yalikuwa yakiitwa mauaji ya kimbari ya Rwanda kama ambavyo imekuwa ikifahamika.
Rwanda imepokea kauli hiyo kwa pongezi kutokana na mauaji hayo kuonekana mara nyingi yakipotoshwa kwa kuyataja kinyume na yalivyokuwa.
Katika mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994, UN inataja idadi ya watu laki nane ndiyo waliuawa huku serikali ya Rwanda ikishikilia watu waliouawa wakati huo walikuwa zaidi ya milioni moja.

Wimbi la wakimbizi wanaokimbia mapigano na ukatili nchini DRC


Wimbi la wakimbizi wanaokimbia mapigano na ukatili nchini DRC kuingia nchini Tanzania kupitia mkoani Kigoma limezidi kuongezeka na sasa inakadiriwa kufikia watu 1,200.

IBADA YA JUMAPILI:


 Rais John Magufuli aliyeambatana na mkewe Janeth Magufuli waliposhiriki ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay,leo Jijini Dar es Salaam.

Baada ya Rais Magufuli, Rais Shein atoa msimamo wake kuhusu muda wa kukaa madarakani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein amesema hayupo tayari kuongeza muda wa uongozi kutoka miaka mitano hadi saba kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya Zanzibar.

Dkt Shein amesisitiza kwamba, aliapa kuilinda katiba ya Zanzibar hivyo hawezi kubadilisha muda wa uongozi na hakuna mtu atakayemfanya abadilishe au amvutie yeye kuendelea kukaa madarakani.

Rais Dkt Shein ameyasema hayo jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baaada ya kurejea kutoka kwenye ziara ya wiki moja katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE) alipokua ameambatana na mke wake, Mama Mwanamwema Shein.

“Mimi naheshimu katiba ya Zanzibar, na nina heshimu sheria za Zanzibar. Muda wangu ukifika nitaondoka haraka sana. Hakuna atakayenilazimisha mimi nikae, au atakayenivutia mimi nikae” alisema Rais Dkt Shein.

Aidha, Dkt Shein amesema kuwa, alisikia wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi wakizungumza hilo, lakini hawazuiwi kujadili kwani wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria, lakini yeye hayuko tayari kuongeza muda.

“Hilo walizungumza wawakilishi barazani, wana haki ya kuzungumza, kwa mujibu wa taratibu zao na sheria zao na yeyote mwingine anaweza kuzungumza. Mimi nilisikia wakati wananzungumza, Mwakilishi mmoja akasema kwamba kuna baadhi ya nchi duniani zina miaka mitano nyingine saba, sasa kwanini na sisi tusiwe na miaka saba!”

Rais Dkt Shein amesema kuwa, suala la miaka saba labda linaweza kuwepo baada ya yeye kutoka lakini hadhani kama kuna jambo kama hilo.

“Mie sijalisema, sitolisema, na hakuna atayanilazimisha niliseme” alihitimisha Rais Dkt Shein, huku akitilia mkazo kwamba, muda wake ukiisha atamchukua mkewe na kumwambia waondoke.

wanafunzi watakiwa kuongeza juhudi ya masomo nchini




wanafunzi kote nchini wametakiwa kufanya biii katika masomo yao ili  kutimiza malengo yao katika maisha  ,rai hiyo imetolewa na  mkurugenzi  wa tasisi binafsi ya wezesha trust fund , lusako mwakiluma  mjini morogoro  , alipotembelea na kufundisha mbinu za kufanikiwa kwa wanafunzi  na stadi za maisha katika sekondari uluguru iliyopo kihonda mjini morogoro .

mkurugenzi huyo amesema kuwa ni vyema wanafunzi wakajitambua nini wanatakiwa kufanya wakiwa katika masomo shuleni badala ya kuingia katika makundi  mabaya , na badaye kujutia makosa.kwa kutotimiza malengo na ndoto zao.
 
''vijana maisha ni nyinyi wenyewe na kama wenyewe amtajikubali na kupambana na hali zenu mkasubiri kusukumwa hakuna litakalotokea''alisema, Madam Lusako nakuongeza kuwa ''kuzaliwa na famiia masikini au kupitia changamoto ni moja katika hali ya maisha ya binadamu yoyote, kijana amua kubadilisha maisha ya familia yako leo kwa kujitambua na kujihakikishia utakuwa wa kwanza katika familia kuondoa umaskini na kufanikiwa sana. Hakuna lisilowezekana kauli mbiu ni (Work Hard, Work Smart then Trust God). alisema lusako mwakiluma.
pia wanafunzi hao wa kidato cha nne katika sekondari ya uluguruWalifundishwa mbinu kumi zenye tija kwa weledi wa hali ya juu. katika kufikia malengo ya kufaulu mitihani yao.

kwa upande wake mwalimu wa shule hiyo bi bukuku amewashukuru wezesha trust fund kwakufika katika shule hiyo na kuweza  kutoa   darasa la stadi   za  maisha kwa wanafunzi hao wa kidato cha nne, nakuwataka  wanafunzi kuzingatia mafunzo hayo ,nakufuata ushauri waliopewa na na taasisi hiyo.

taasisi hiyo binafi ya wezesha trust imekuwa ikisaidia wanafunzi wenye mazingira magumu katika mkoa  wa morogoro  na mengine nchini tanzania .