wanafunzi kote nchini wametakiwa kufanya biii katika masomo yao ili kutimiza malengo yao katika maisha ,rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa tasisi binafsi ya wezesha trust fund , lusako mwakiluma mjini morogoro , alipotembelea na kufundisha mbinu za kufanikiwa kwa wanafunzi na stadi za maisha katika sekondari uluguru iliyopo kihonda mjini morogoro .
mkurugenzi huyo amesema kuwa ni vyema wanafunzi wakajitambua nini wanatakiwa kufanya wakiwa katika masomo shuleni badala ya kuingia katika makundi mabaya , na badaye kujutia makosa.kwa kutotimiza malengo na ndoto zao.
''vijana maisha ni nyinyi wenyewe na kama wenyewe amtajikubali na
kupambana na hali zenu mkasubiri kusukumwa hakuna litakalotokea''alisema, Madam
Lusako nakuongeza kuwa ''kuzaliwa na famiia masikini au kupitia changamoto ni
moja katika hali ya maisha ya binadamu yoyote, kijana amua kubadilisha
maisha ya familia yako leo kwa kujitambua na kujihakikishia utakuwa wa
kwanza katika familia kuondoa umaskini na kufanikiwa sana. Hakuna
lisilowezekana kauli mbiu ni (Work Hard, Work Smart then Trust God). alisema lusako mwakiluma.
pia wanafunzi hao wa kidato cha nne katika sekondari ya uluguruWalifundishwa mbinu kumi zenye tija kwa weledi wa hali ya juu. katika kufikia malengo ya kufaulu mitihani yao.
kwa upande wake mwalimu wa shule hiyo bi bukuku amewashukuru wezesha trust fund kwakufika katika shule hiyo na kuweza kutoa darasa la stadi za maisha kwa wanafunzi hao wa kidato cha nne, nakuwataka wanafunzi kuzingatia mafunzo hayo ,nakufuata ushauri waliopewa na na taasisi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni