Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed
Shein amesema hayupo tayari kuongeza muda wa uongozi kutoka miaka mitano
hadi saba kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya Zanzibar.
Dkt
Shein amesisitiza kwamba, aliapa kuilinda katiba ya Zanzibar hivyo
hawezi kubadilisha muda wa uongozi na hakuna mtu atakayemfanya
abadilishe au amvutie yeye kuendelea kukaa madarakani.
Rais
Dkt Shein ameyasema hayo jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari mara baaada ya kurejea kutoka kwenye ziara ya wiki moja katika
nchi za Falme za Kiarabu (UAE) alipokua ameambatana na mke wake, Mama
Mwanamwema Shein.
“Mimi
naheshimu katiba ya Zanzibar, na nina heshimu sheria za Zanzibar. Muda
wangu ukifika nitaondoka haraka sana. Hakuna atakayenilazimisha mimi
nikae, au atakayenivutia mimi nikae” alisema Rais Dkt Shein.
Aidha,
Dkt Shein amesema kuwa, alisikia wawakilishi katika Baraza la
Wawakilishi wakizungumza hilo, lakini hawazuiwi kujadili kwani wanafanya
hivyo kwa mujibu wa sheria, lakini yeye hayuko tayari kuongeza muda.
“Hilo
walizungumza wawakilishi barazani, wana haki ya kuzungumza, kwa mujibu
wa taratibu zao na sheria zao na yeyote mwingine anaweza kuzungumza.
Mimi nilisikia wakati wananzungumza, Mwakilishi mmoja akasema kwamba
kuna baadhi ya nchi duniani zina miaka mitano nyingine saba, sasa
kwanini na sisi tusiwe na miaka saba!”
Rais
Dkt Shein amesema kuwa, suala la miaka saba labda linaweza kuwepo baada
ya yeye kutoka lakini hadhani kama kuna jambo kama hilo.
“Mie sijalisema, sitolisema, na hakuna atayanilazimisha niliseme” alihitimisha Rais Dkt Shein, huku akitilia mkazo kwamba, muda wake ukiisha atamchukua mkewe na kumwambia waondoke.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni