Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi, Joseph Kakunda ameagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Njombe kufanya uchunguzi wa matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Viziwi Njombe.
Katika
matokeo yaliyotangazwa jana Jumanne Januari 30,2018 na Baraza la
Mitihani la Tanzania (Necta), shule hiyo katika matokeo ya mtihani
uliofanyika Oktoba na Novemba mwaka jana watahiniwa wote 21 wamepata
daraja sifuri (0).
Naibu
Waziri Kakunda ametoa agizo la kufanyika uchunguzi leo Jumatano Januari
31,2018 bungeni alipojibu swali la mbunge wa Buyungu (Chadema), Samson
Bilago.
Bilago alitaka kujua ni kwa nini shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu zinafanya vibaya kwenye mitihani.
Akizungumzia
hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, George Mkuchika amesema walimu waliosoma elimu maalumu
watapata ajira bila kikwazo cha kusubiri.
Mkuchika amesema wanasubiri kupelekewa orodha ya walimu hao.
Alikuwa
akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini
aliyetoa mfano wa shule ya Viziwi Njombe ya wanafunzi wa mahitaji
maalumu iliyofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne
akisema ni kutokana na kukosa walimu hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni