Kijana
Emmanuel Ernest wa kitongoji cha Ilolo, Mvumi Misheni wilaya ya
Chamwino Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo
huku mwingine akijeruhiwa vibaya baada ya tembo huyo kuvamia mashamba ya
zabibu.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema tembo huyo alikuwa akitafuta maji majira ya
alfajiri hivyo baadhi ya wanakijiji baada ya kumuona walikusanyika na
kupiga mayowe, kitendo kilichomfanya mnyama huyo kukasirika na kuanza
kuwafukuza kabla ya kumkuta marehemu Emanuel akiwa na mdogo wake
wakichimba mitaro ya mizabibu na kumkanyaga kifuani na kumvunja mbavu
nne na kusababisha kifo chake.
Kaimu
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mvumi Misheni, Peter Songoro,
amethibitisha kupokea majeruhi wawili, akiwemo marehemu na mdogo wake
Amani Joseph ambaye alikanyagwa mgongoni na kisha utumbo kutoka nje,
kabla ya Emmanuel kufariki baadaye wakati akipatiwa matibabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni