Msanii wa Bongo Flava, Matonya ameelezwa kushangazwa na WCB kutoa wimbo ‘Zilipendwa’ jina ambalo ameshalitumia katika ngoma yake.
Kupitia mtandao wa Instagram Matonya ametoa pongezi kwa kile kilichofanyika ila hajapendezwa na kitendo cha kutokupewa taarifa hadi ngoma hiyo kutoka kwani ana haki zake katika jina hilo.
Nduguzangu wasafi / Nawapongeza sana kwa kazi mzuri mnazo zifanya / Nilifurahi Sana mlichokifanya kwa saida karoli dadaetu/ mlimuita mkamshirikisha akawapa Baraka zake/ kwangu mlishindwa nini? Sina shida Ya Pesa nina shida Ya heshima cose najua dunia ni mapito/ kama mimi naibiwa haki yangu vipi wasanii wachanga? Basata mkowapi? Wadau Wa muziki mkowapi? Usipo ziba ufa tajenga kuta!! Khaaa tena Bila woga lakini haki itafata mkondo wake.Hapo jana wasanii wote wa WCB yaani Diamond Platnumz, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Lava Lava, Harmonize na Maromboso aliungana kwa pamoja na kutoa wimbo ‘Zilipendwa’ ambao kwa sasa umekuwa gumzo kila kona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni