Jumapili, 27 Agosti 2017

Masau Bwire anunuliwa maji na mashabiki wa Simba



 Pamoja na majigambo yake, mashabiki wa Simba waliamua kumnunulia maji Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ili kumpoza machungu.

Simba imeitwanga Ruvu Shooting kwa mabao 7-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni siku chache baada ya mwalimu huyo kitaaluma ambaye ni msemaji wa timu hiyo ya jeshi kusema Simba ni toy au mwanasesere.

Mashabiki hao waliamua kumnunulia Masau maji ya kunywa na kumpelekea kwenye gari la wachezaji wa timu ya Ruvu.

Kabla ya hapo, wengi waliamua kupiga naye picha wakimvisha kofia za Simba na wengine wakimshangilia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni