Jumapili, 27 Agosti 2017

Floyd Mayweather amtwanga McGregor kwa TKO




Mayweather kulia akimtwanga sumbwi la ushindi McGregor kwenye raundi ya 10 ya pambano.

 Bondia maarufu zaidi duniani, Floyd Mayweather ameendeleza ubabe kwenye mchezo huo kwa kumtwanga Knock Out  bingwa wa UFC Conor McGregor kwenye mchezo wa ubingwa.



Katika raundi ya kwanza na ya pili, McGregor alionekana kumzidi Mayweather huku refa akamuonya kutokana na aina ya upigaji wake ambapo alionekana kumpiga Mayweather chini ya kichwa.
Baada ya raundi ya 3 na ya 4 kuisha McGregor alionekana kuchoka na raundi zilizobakia zote alidundwa  mpaka ilipofikia raundi ya 10 alipopigwa TKO zikiwa zimesalia raundi mbili kumalizika kwa pambano.
Ushindi wa leo wa Mayweather umeweka rekodi nzuri kwake ambapo mpaka sasa anakuwa amecheza mapambano 50 ya mashindano bila kupigwa huku akishinda kwa TKO mechi 26.
Baada ya mchezo huo Floyd amewashukuru mashabiki wake kwa kusema amewapa kile walichokuwa wakisubiria kwa muda mrefu na kutangaza kustaafu rasmi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni