Jumapili, 27 Agosti 2017

Lipuli ilivyoikazia Yanga na Tshishimbi akiwemo




Leo Agosti 27, ilipigwa Mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu kati ya Yanga na Lipuli FC katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam huku mabingwa wa tetezi wa ligi kuu Tanzania bara wakilazimisha sare ya goli 1-1 katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi walionekana kushindwa kuonyesha mbwembwe zao dhidi ya Lipuli ambao ndio kwanza wamerudi katika ligi kuu baada ya kupotea kwa kushuka daraja miaka kadhaa iliyopita.
Katika mchezo huo kinara wa Lipuli Seif Abdallah aliing'arisha timu yake kwa kuipatia Goli la kwanza dakika 44 kabla ya Donald Ngoma hajasawazisha goli hilo dakika ya 46 lilodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Akizungumza baada ya mchezo huo Seif Abdallah amesema "Nina furaha sana kufunga goli langu la kwanza baada ya kurudi kwenye ligi kuu. Huu ni muendelezo wa rekodi yangu kila ninapokutana na Yanga" 
Pamoja na hayo Lipuli wamepata doa baada ya kucheza pungufu dakika za majeruhui baada ya Nahodha wa timu hiyo Asante Kwasi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na maamuzi yaliyotolewa na refa qwa mchezo.
Kuhusu msimamo wa raundi ya kwanza Simba SC wanaongoza kwa magoli 7 na pointi 3 nafasi ya 1 huku watani zao yanga wakiwa nafasi ya 9, pointi 1 na goli 1.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni