Ijumaa, 2 Februari 2018

picha za maadhimisho ya wiki ya sheria mkoa wa morogoro

watumishi wa mahakama mkoani morogoro wametakiwa kujifunza matumizi ya kompyuta  ili kurahisisha kazi za muhimili huo, nakuingia katika mfumo wa tehama.

hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa morogoro   Dk Steven Kebwe katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria  ngazi ya mkoa , iliyofanyika manispaa y morogoro.


dk kebwe ambaye alikuwa  mgeni rasmi alionya  watumishi wa mahakama kuachana na vitendo vya rushwa ili kutoa haki kwa raia. sambasamba na raia kutojichukulia sheria mikononi .













Duh!! Zari kafikia huku juu ya Diamond Platnumz

Ni siku chache zimepita toka msanii Diamond Platnumz kudaiwa kutoka kimapenzi na wasichana wengine tofauti na mama watoto wake Zari the bosslady.
Inasemekana kuwa Diamond Platnumz hupeleka wasichana tofautitofauti nyumbani kwake Madale, kutokana na tetesi zilizokuwa zikiendelea kwenye mitandao ya kijamii ikaonekana Zari kukasirishwa na tabia hiyo.

Hivyo kupitia instagram account ya Zari ameonekana kumu’unfollow baba watoto wake Diamond Platnumz, kitu hiki kimeleta maswali mengi kwa baadhi ya mashabiki na wengi kuhusisha ukaribu uliotokea kati ya Wema Sepetu na Diamond siku ya uzinduzi wa kutambulisha rasmi Marombosso WCB.

: JPM kateua Mwanasheria Mkuu mpya

February 1, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo amemteua Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Pia President JPM amemteua Paul Joel Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG) kuanzia February 1, 2018.

 Balozi John Kijazi akitangaza uteuzi huu mpya na nafasi walizopangiwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu George Masaju na Naibu wake Gerson Mdemu.

Alhamisi, 1 Februari 2018

Kambale asimamishwa Singida United


Kampuni ya TTCL imefutwa na kuwa Shirika



 Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya (TTCL), imefutwa na kubadilishwa kuwa Shirika (TTCL Corporation).
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam katika makao makuu ya shirika hilo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa, amesema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuona wa kuwa na shirika la mawasiliano madhubuti kwa ajili ya kuleta maslahi mapana ya nchi, huku akitoa shukrani pia kwa Wabunge wote kwa kukubali kupitisha muswada huo.
Aidha Prof Mbarawa, amesema uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano unatoa fursa ya kuboresha sekta kwa kuweka mazingira mazuri ya usimamizi wa miundombinu ya mikakati chini ya shirika hilo.
Profesa Mbarawa pia amewajulisha Watanzania wote kuwa mabadiliko ya kuhama kutoka kampuni kuwa shirika la mawasiliano hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zinatolewa na kampuni ya simu ya (TTCL) huku akielezwa kuwa wanaodaiwa na iliyokuwa kampuni hiyo watatakiwa kulia madeni yao kama mikataba yao inavyosema na wanaoidai watalipwa pia.

Emmanuel Okwi: Simba bado ina kazi ngumu


 Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amesema pamoja na Simba kuendelea kuongoza lakini bado wana kazi ngumu kutokana na ushindani wa ligi ulivyo.

Simba inaongoza Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya pointi tano tofauti ya Azam FC wanaoshika nafasi ya pili.

Okwi amesema wanaamini wako katika nafasi nzuri lakini lazima wafanye juhudi zaidi.

“Tunaongoza ligi kwa sasa, lakini utaona tofauti ni ndogo sana na anayetufuatia. Maana yake kama timu tunatakiwa kuendelea kupambana hadi mwisho.

“Ushindani ni mkali sana, kila timu inataka kufanya vizuri na sisi tunataka kufanya vizuri. Tumekuwa tukijituma kama timu kwa faida ya klabu yetu na tunajua bado tunatakiwa kujituma,” alisema.

Okwi ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na 12.

Mara nyingi anapohojiwa Okwi amesema kitu cha kwanza kwake ni timu kwa kuwa kama mchezaji yeye na wenzake wamekuwa wakipigana kwa ajili ya timu.

JPM asema “Nitachukua hatua, tena mwezi huu wa pili hautaisha”

Rais John Magufuli leo February 1, 2018 katika Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Mahakama amesema yupo tayari kufanya uteuzi wa majaji wengine ili kukabiliana na changamoto ya upungufu mkubwa wa majaji ambayo inasababisha mrundikano wa mashauri katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.
Tofauti na hilo Rais Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kuendelea kurekebisha dosari ambazo zimekuwa zikiuchafua mhimili huo wa Dola ikiwemo Majaji na Mahakimu kujihusisha na vitendo vya upokeaji wa rushwa na ucheleweshaji wa kesi ambavyo vinasababisha hasara kubwa kwa taifa.
Aidha amempongeza Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma kwa hatua ya kuwafukuza kazi watumishi 112 wa Mahakama wakiwemo Mahakimu 17 waliojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili
Rais Magufuli pia ameeleza kushangazwa na vyombo vingine ambavyo hushirikiana na Mahakama kama vile Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Magereza na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa kutowawajibisha watumishi wake wanaokiuka maadili.
“Mwaka jana nililalamika, sasa mwaka huu sitalalamika, nitachukua hatua, tena mwezi huu wa pili hautaisha, pale ofisini kwangu napokea barua nyingi za malalamiko ya ucheleweshaji wa kesi, kila kesi upelelezi haujakamilika, ni lazima kuwe na utatuzi wa jambo hili” – Rais Magufuli
“Hivi sasa kuna kesi za Shilingi Bilioni 169.1 na Dola za Marekani Milioni 38.2 zinasubiri tu na nchi inakosa mapato” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.” – Rais Magufuli

Serikali ya Kenya yashtakiwa kwa kufungia vituo vya TV kwenye ‘kuapishwa’ Raila

Mwanaharakati nchini Kenya Okiya Omtatah amefungua mashtaka dhidi ya serikali katika Mahakama Kuu kutokana na uamuzi wake wa kuzima vituo vya televisheni vya Citizen TV, NTV na KTN pamoja na Inooro TV siku ya ‘kujiapisha’ Kiongozi wa Upinzania NASA Raila Odinga.
Omtatah ameeleza kuwa kufungiwa kwa vyombo hivyo vya habari  ni kinyume cha sheria na hakuna sheria yoyote iliyowapa mamlaka ya kutekeleza suala hilo.
Amedai kuwa serikali hiyo lazima izuiwe katika kudharau utawala wa sheria jambo ambalo ni msingi mkuu wa thamani ya taifa na kanuni ya utawala.
Ameongeza kuwa anahitaji mahakama iamuru serikali ilipe fidia vyombo hivyo vya habari vilivyofungwa na kusababishiwa hasara kutokana na jambo hilo.

Wabunge waomba mkataba Mlimani City uchunguzwe

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeliomba Bunge kumuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa mchakato wa mikataba yote ya mradi wa Mlimani City.

Akiwasilisha bungeni leo Februari1, 2018 taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka amesema kamati hiyo imebaini dosari katika mkataba wa uendeshaji wa mradi huo, kusababisha Serikali kukosa mapato.

Miongoni mwa dosari alizozitaja za mradi huo ni kukiukwa kwa sheria ya Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) inayotaka ili kibali cha uwekezaji kutolewa lazima mwekezaji alete ushahidi kuwa na mtaji wa kutosha.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kilikodisha eneo hilo kwa kampuni ya Mlimani Holding Ltd.

Hivi karibuni PAC ilifanya ziara katika eneo la Mlimani City na kuutaka uongozi wa UDSM kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani City Holding Ltd kutokana na mapungufu yaliyojitokeza, huku ikihoji sababu ya mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 tu.

Licha ya kutotaja siku, Kaboyoka amesema mara ukaguzi huo utakapokamilika taarifa yake iwasilishwe bungeni.

Mwananchi:

FAO yatoa msaada kwa Tanzania kupambana na viwavi jeshi






Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo wamesaini mkataba wa ushirikiano wenye lengo la kuisaidia Tanzania kujenga uwezo wa kufuatilia na kudhibiti uvamizi wa viwavi jeshi hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya makubaliano hayo mkoani Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Mhandisi Mathew Mtigumwe, amesema  makubaliano hayo  yamekuja kwa wakati muafaka ambapo Serikali ilikuwa inachukua hatua mbali mbali kukabiliana na tatizo hilo.

Mwakilishi Mkazi wa FAO,Fred Kafeero,amesema  Shirika hilo limekuwa likifanya kazi pamoja na Serikali katika nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo Tanzania kudhibiti athari inayosababishwa na viwavi jeshi hivyo.

Kupitia makubaliano hayo,FAO itatoa msaada wa kiutaalamu na kifedha wenye thamani ya Dola za Kimarekani 250,000 ambazo ni zaidi ya Tshs. Milioni 550 kuimarisha ufuatiliaji na kukuza uelewa kuhusu  viwavi jeshi kwa mazao kabla na wakati wa misimu ya kilimo ijayo.

TANZIA: Radio wa Goodlife afariki dunia

Muimbaji kutokea kwenye kundi la Good Lyfe Moses Sekibooga ambaye wengi wanamfahamu Radio kutokea Uganda imeripotiwa amefariki dunia asubuhi ya leo February 1,2018 baada ya kukaa ICU kwa siku kadhaa zilizopita, hii ni baada kuripotiwa kupata ajali ya gari  January 23,2018.




 Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel,  tangu January 23 mwaka huu hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi wa klabu.
Hapo jana Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya  matibabu ya msanii huyo, pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la Light the World.
 


Radio
Muimbaji Radio ameacha pengo kubwa katika kundi la Good Lyfe ambalo liliundwa na yeye mwenyewe pamoja na Weasel ambaye ni mdogo wa muimbaji na legend wa muziki nchini Uganda Joseph Mayanja ambao wengi tunamfahamu kama Jose Chameleon.


Kutoka kushoto ni marehemu Radio akiwa na mwenzake Weasel
Taarifa za kifo cha Radio zinakuja ikiwa ni siku moja imepita toka Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuripotiwa kutoa milioni 30 kama mchango kwa ajili ya kuokoa maisha ya staa huyo kwa kugharamia matibabu.
Radio na Weasel wamefanya nyimbo nyingi ambazo zimewahi pia kupata Air time katika TV  na Radio Stations za Tanzania, Don’t Cry ft Wizkid, Zuena na wimbo wa Where You Are waliokuwa wameshirikishwa na Blu 3 na huu uliwafanya wajulikane zaidi Tanzania kutokana na wimbo huo kufanya vizuri.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 1


Dar yakosekana katika mikoa 10 iliyofanya vizuri



   Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetoa mpangilio wa ubora wa ufaulu kimikoa wa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017, huku Dar es Salaam ukikosekana katika mikoa 10 iliyofanya vizuri.

Hata hivyo, mkoa huo umepanda kutoka nafasi ya 18 mwaka juzi, hadi nafasi ya 16 mwaka jana. Katika orodha hiyo mkoa wa Kilimanjaro umepanda kutoka nafasi ya tano mwaka 2016 hadi nafasi ya kwanza mwaka jana.

Mkoa wa Pwani nao umepanda kutoka nafasi ya saba mwaka juzi hadi nafasi ya pili mwaka jana. Katika orodha hiyo Tabora imeshika nafasi ya tatu kutoka nafasi ya 10 mwaka 2016.

Mikoa mingine iliyofuata na nafasi iliyoshika ni Shinyanga (nafasi ya nne kutoka nafasi ya tisa), Mwanza (nafasi ya tano kutoka nafasi ya sita).

Mkoa wa Njombe uliokuwa kwa kwanza mwaka 2016, mwaka jana umeporomoka hadi nafasi ya 15.

Mkoa wa Iringa ulishika nafasi ya pili mwaka 2016, lakini mwaka jana umeporomoka hadi nafasi ya 17 huku Kagera ulioshika nafasi ya tatu, ukishuka hadi nafasi ya tisa.

Mkoa ulioshika mkia katika mpangilio huo ni Kaskazini Unguja uliotoka nafasi ya 29 mwaka juzi hadi nafasi ya 31 mwaka jana, ukifuatiwa na Kusini Unguja ulioshika nafasi ya 30 ambayo pia uliishika mwaka juzi.

Mikoa mitano iliyoshika mkia ni Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba, Kusini Pemba na Lindi.