
Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya (TTCL), imefutwa na kubadilishwa kuwa Shirika (TTCL Corporation).
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam katika makao
makuu ya shirika hilo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa,
amesema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuona
wa kuwa na shirika la mawasiliano madhubuti kwa ajili ya kuleta maslahi
mapana ya nchi, huku akitoa shukrani pia kwa Wabunge wote kwa kukubali
kupitisha muswada huo.
Aidha Prof Mbarawa, amesema uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano
unatoa fursa ya kuboresha sekta kwa kuweka mazingira mazuri ya usimamizi
wa miundombinu ya mikakati chini ya shirika hilo.
Profesa Mbarawa pia amewajulisha Watanzania wote kuwa mabadiliko ya
kuhama kutoka kampuni kuwa shirika la mawasiliano hayatawaathiri kwa
namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zinatolewa na
kampuni ya simu ya (TTCL) huku akielezwa kuwa wanaodaiwa na iliyokuwa
kampuni hiyo watatakiwa kulia madeni yao kama mikataba yao inavyosema na
wanaoidai watalipwa pia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni