Taarifa
zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umewaandikia barua TFF
kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza
June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam.
Sababu
za msinngi zilizofikia Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi
ya michunao ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia
FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi.
Kutokana
na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema
kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri
kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM
Alger pia Rayon Sports ya Rwanda.
Taarifa
hizo zinazoelezwa kutoka Yanga kupitia viongozi wa Kamati ya Utendaji
wa klabu hiyo, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na
muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao.
Kufuatia
kuandika barua hiyo ya kuomba kujiondoa, Yanga wanakuwa wameikwepa
Simba kwenye mashindano ambapo walikuwa wamepangwa pamoja na mabingwa
hao wa Ligi Kuu Vodacom.
Simba
na Yanga zimepangwa pamoja kwenye kundi C ambapo kuna timu zingine
ambazo ni Dakadaha ya Somalia pamoja na St. George kutoka Ethiopia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni