Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe,
amewapongeza Simba kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya
SportPesa Super Cup nchini Kenya.
Simba
imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya ushindi wa changamoto ya mikwaju
ya penati wa mabao 5-4 dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC ikiwa ni baada ya
dakika 90 kumalizka kwa sare tasa ya 0-0.
Akizungumza
bungeni mjini Dodoma, Mwakyembe amefunguka na kueleza Simba
wamethibitisha kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom si kwa kubahatisha
mpaka kufikia hatua hiyo ya kucheza fainali na Gor Mahia.
"Napenda
kuchukua fursa hii kuwapongeza Simba kwa kufanikiwa kutinga fainali ya
SportPesa Super Kenya, wamethibitisha kuwa walichukua ubingwa wa ligi si
kwa kubahatisha kwa soka la kiwango" amesema.
Mchezo
wa fainali ya mashindano hayo utachezwa kwenye Uwanja uleule wa Afraha
Jumapili ya wiki hii ambapo bingwa wa michuano hiyo atacheza dhidi ya
Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park nchini England.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni