Kwesi Nyantakyi amekamatwa akipokea $65,000 ambazo ni zaidi ya Tsh. Milioni 148 kutoka kwa Mwandishi habari mpelelezi aliyejifanya kuwa mfanyabiashara mwenye hamu kubwa ya kuwekeza katika soka nchini Ghana.
Mpaka sasa, Nyantakyi ambaye pia ni Afisa wa pili kwa uwezo katika soka la Afrika hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo.
Waziri wa habari Mustapha Abdul-Hamid, amesema Serikali imekivunja chama cha soka Ghana GFA, kutokana na muozo ulionekana na hatua za muda za kuongoza soka zitatangazwa hivi karibuni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni