mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Alhamisi, 7 Juni 2018
Watu 10 katika ndege iliyopotea wamefariki
Leo June 7, 2018 Ndege ndogo ya Kampuni ya FlySax iliyokuwa imeripotiwa kutoweka katika anga ya Kenya jumanne jioni imepatikana huku abiria wote 8, kapteni pamoja na afisa wa ndege hiyo kuripotiwa kufariki.
Mwenyekiti wa Kampuni ya FlySax, Charles Wako ameutangazia umma wa Kenya mchana wa leo kuhusiana na vifo hivyo vilivyotokea baada ya ndege hiyo kuanguka.
Ndege ndogo aina ya Cessna C208 iliripotiwa kutoweka ilipokuwa inatokea katika eneo la Kitale kuelekea uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na kupatikana ikiwa imeanguka katika msitu wa Aberdares katika kaunti ya Nyandarua nchini Kenya.
Duru za kuaminika zinasema kuwa ndege hiyo ilikutana dhoruba kali iliyosababisha kuanguka kwa ndege hiyo.
Aidha majina ya watu waliokuwemo kweneye ndege hiyo ni Barbra Wangeci Kamau (kapteni), Jean Mureith (afisa wa ndege), Ahmed Ali Abdi, Karaba Sailah Waweru Muiga, Khetia Kishani, Matakasakarai Thamani, Matakatekei Paula, George Ngugi Kinyua, Pinuertorn Ronald na Robinson Wafula ambao wote hao walikuwa ni abiria.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni