Alhamisi, 7 Juni 2018

Alichofanya Trump kwa Waislamu kwa mara kwanza toka aingie Ikulu

Leo June 7, 2018 Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara ya kwanza tangu kuingia ofisini alifuturu pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu katika ikulu ya White House.
Ingawa White House haijatoa orodha kamili ya wageni walioalikwa kwenye hafla hiyo, waandishi wa habari waliohudhuria wamedokeza kwamba wengi wa waliokuwepo walikuwa maafisa wa serikali na mabalozi wa nchi za Kiislamu.
Ni mara ya kwanza kwa Trump kufuturu na waislamu White House baada ya kuepuka zoezi hilo mwaka jana. Kwa miongo kadhaa imekuwa kama desturi kwa marais wa Marekani kufuturu na waislamu katika ikulu wakati wa Ramadhan.
Licha ya hatua ya Trump ya kualika waumini wa dini ya Kiislamu kufuturu kwenye ikulu, mamia ya watu walikusanyika nje ya White House kupinga rais huyo kwa sera na matamshi mabaya dhidi ya dini ya Kiislamu wakati wa kampeni na hata wakati wake kama rais.
Rais huyo pia amekemewa kwa kupitisha marufuku ya usafiri dhidi ya wasafiri wanaotoka nchi za Kiislamu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni