Droo ya upangaji wa makundi kwa timu 16 zitakazoshiriki ligi ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) ijulikanayo kwa jina la #UhaiCup imefanyika leo ndani ya studio za #AzamTV.
Ligi hiyo inayoanza rasmi Juni 9, mwaka huu katika viwanja vya Chuo
Kikuu cha Dodoma jijini Dodoma itashirikisha timu za vijana wenye umri
huo kutoka katika vilabu vilivyoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu
uliomalizika hivi karibuni.Matokeo ya droo hiyo iliyoongozwa na Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo ni kama ifuatavyo:-
Kundi A: Yanga, Ruvu Shooting, Mbeya City, Mbao FC.
Kundi B: Simba, Singida United, Stand United, Njombe Mji.
Kundi C: Azam, Mtibwa Sugar, Mwadui FC, Majimaji FC.
Kundi D: TZ Prisons, Lipuli FC, Kagera Sugar, Ndanda FC.
Azam TV ambao ni wadhamini wa ligi hiyo kwa upande wa matangazo ya Televisheni, itakurushia mechi zote mbashara, ambapo kwa mujibu wa ratiba, kutakuwa na mechi mbili kila siku, ya kwanza ikianza saa 8:00 mchana na mechi ya pili ikianza saa 10:00 jioni.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni