Alhamisi, 7 Juni 2018

VIONGOZI MATAWI YANGA WATOA MAAZIMIO YA MKUTANO, NI MABADILIKO NA YUSUPH MANJI, MWAKYEMBE AKARIBISHWA


Kuelekea mkutano Mkuu wa Yanga utakaofanyika Juni 10 2018, haya ni maadhimio mkutano wa matawi ya Yanga yaliyofanyika jana.

1. Kwa pamoja viongozi wa matawi wamekubaliana kwenda kwenye mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji. Kabla ya kuibadilisha klabu kwanza wanachama wenyewe tuanze kubadilika kifikra. Aidha tuwahamasishe wanachama kufika kwa wingi kwenye Mkutano Mkuu. Kila mmoja ahakikishe kadi yake ipo hai.

2. Wadhamini chini ya Mkuchika, Jaji Mkwawa, Francis Kifukwe na Mzee Jabir Katundu walikaa na Kaimu Mwenyekiti kujadili Mkutano Mkuu na mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu. Kesho tarehe 7 (ambayo ni leo) wanakutana na Yusuf Manji.


3. Tunataka kwenda kwenye mabadiliko tukiwa na uwezo wa kulipa wachezaji mishahara, kusajili wachezaji wazuri na tuwe na timu imara yenye ushindani.

4. Kamati ya mabadiliko itatoa taarifa yake mbele ya wanachama wa Yanga siku ya Mkutano Mkuu.
5. Mkutano huo utahudhuriwa na Waziri Mwakyembe, Mh. Mkuchika na viongozi wote waandamizi wa serikali wadau wa Yanga.
6. Mabango ya aina yoyote hayaruhusiwi na watu wabishane kwa hoja bila mizozo.
6. Kauli mbiu ya viongozi wa Matawi ni 'Mabadiliko na Yusuph Manji.
7. Mabadiliko yatawezekana iwapo wanayanga tutaacha unafiki na kuwa na umoja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni