Na Mwandishi Wetu, Nakuru
Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre
leo atakuwa jukwaani Simba ikicheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la
SportsPesa Super Cup.
Wakati Simba ikijiandaa kucheza mechi hiyo leo saa 7 mchana, Lechantre anaonekana yuko jukwaani.
Simba itaivaa Kakamega Homeboyz katika mechi ya nusu fainali ya SportPesa Super Cup kwenye Uwanja wa Afrah, mjini hapa.
Taarifa zinaeleza, kuna mgomo baridi kutoka kwake na msaidizi wake, Mohamed Habibi.
Hivyo Simba itaingozwa na Masoud Djuma, msaidizi ambaye Lechantre alimkuta ameishaanza kazi na kikosi hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni