Jumanne, 5 Juni 2018

Singida United watinga nusu fainali, AFC Leopard nje

Michuano ya SportPesa Super Cup imeendelea tena leo Nakuru nchini Kenya kwa club ya Singida United kucheza na AFC Leopard katika mchezo wa mtoano.

Singida United ambao wameingia katika mchezo huo wakiwa makini kutokana game yao ya FA kuruhusu magoli dhidi ya Mtibwa, hata hivyo leo haikuwa rahisi kwa timu zote kupata goli hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yalikuwa 0-0.

Baada ya hapo game ikaamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Singida United wakafanikiwa kuingia nusu fainali kwa ushindi wa penati 4-2, hivyo sasa watacheza dhidi ya Gor Mahia katika mchezo wa nusu fainali baada ya kuwatoa Leopard.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni