Jumanne, 5 Juni 2018

Maxcom yafunguka aliyesababisha Mgomo wa wafanyakazi na hasara Milioni 80

Leo June 5, 2018 Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma kutoka kampuni ya Maxcom wametolea ufafanuzi suala la kuosekana kwa huduma ya tiketi za kielektroniki kwenye baadhi ya vituo vya mabasi ya mwendokasi.
Katika taarifa hiyo Maxcom wamekiri kuwa kumekuwepo upungufu  wa watoa huduma yaani wakatisha tiketi baadhi ya vituo vya mabasi nakusema jambo hilo lilisababishwa na UDA-RT kukaidi kuwalipa mishahara wakatisha tiketi.
AyoTV na millardayo.com tumeipata taarifa iliyosainiwa na Deogratius Lazari kutoka kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Maxcom Africa PLC .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni