Simba Sports Club imekuwa mbele katika kuanzisha vitu vipya kwa kukuza ufanisi na morali za wachezaji wake.
Ikumbukwe kuwa Simba SC ndiyo ilikuwa ya kwanza kuwa na tunzo za wachezaji wake kila mechi na kila mwezi.
Mo
Simba Award zimeanzishwa na Mwekezaji katika klabu ya Simba SC,
Mohammed Dewji kwa lengo la kutoa zawadi kwa wanafamilia wa Simba ambao
wamesaidia klabu kupata mafanikio kwa msimu wa 2017/2018.
Tuzo hizi zitakuwa na vipengele 17 ambavyo vitahusisha wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, mashabiki na wasimamizi wa mchakato wa mabadiliko.
Sherehe za kuwakabidhi zawadi washindi zitafanyika mwezi huu wa Juni 2018.
Imetolewa na Idara ya Habari, Simba SC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni