Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni
(Mstaafu), George Mkuchika amewataka wasioridhishwa na utendaji kazi wa
Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kwenda mahakamani kutafsiri sheria.
Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA), Ruth Mollel akiihoji serikali leo Bungeni
Mkuchika ametoa kauli hiyo, leo Juni 8, 2018 Bungeni jijini Dodoma
wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA), Ruth Mollel
aliyeihoji serikali kuwa, Wakurugenzi wa Halmashauri ambao
wameteuliwa wengi wao walikuwa ni wana CCM walioshindwa katika kura za
maoni na wao ndio wasimamizi wa uchaguzi kuna wengine kama huyu wa
Ubungo anahudhuria vikao vya CCM, Swali langu ikiwa tutaleta orodha ya
Wakurugenzi ambao tunajua ni wana CCM na walikuwa katika kura za maoni
Je serikali itakuwa tayari kuwaondoa?
“Swali la pili tunao wakuu wa mikoa ambao wanalipwa kwa pesa
za walipa kodi Watanzania wenye vyama na wasiokuwa na vyama lakini wengi
wameonyesha itikadi za kisiasa ukiangalia mkuu wa mkoa Arusha, Mkuu wa
Mkoa wa Manyara na wengine Je, serikali ina kauli gani kuhusu hilo?
Akijibu swali hilo, Mkuchika amesema kuwa “Mkurugenzi yoyote utakaye
mchagua katika nchi hii lazima kuna Chama anachokipenda, huyu yuko pale
baada ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi na Waraka wa utumishi wa umma unasema
Mtumishi wa umma anaeteuliwa na Rais endapo hata ridhia kufanya ile
kazi ana ruksa ya kumuambia Mh. Rais naomba niendelee na kazi yangu ,
sasa hao wakurugenzi walipokuwa wanafanya kazi walishakoma kazi
waliokuwa wanaifanya, kazi wanayoifanya ni Ukurugenzi wa Halmashauri
nataka niseme Rais anapoingia madarakani anapanga safu yake.”
Ameongeza, “Yule wa Ubungo kuhudhuria vikao naomba nisema mkishakuwa
mnachama tawala siku zote kazi yenu nikuihoji serikali , Mkurugenzi wa
Ubungo sio Mjumbe wa CCM lakini anweza kutwa akaelezea utendaji wa ilani
ya uchaguzi katika jimbo la Ubungo.”
Amesisitiza kuwa “Swali la pili kuhusu wakuu wa mikoa , nataka niseme
Wakuu wa Mikoa wanamuwakilisha Rais, Mkuu wa Mkoa ndio Rais wa Mkoa ule
, Rais ni neno la kiarabu maana yake kichwa kwahiyo kichwa cha mkoa ule
ni Mkuu wa mkoa ule, huyu Mkuu wa Mkoa anamuwakilisha Rais , hutegemei
huyu Mkuu wa mkoa afanya mambo tofauti anayofanya Rais, lakini mwisho
nimalizie kusema kwamba nchi hii tunachombo kinaitwa mahakama muhimili
wa mahakama kazi yake ni kutafsiri sheria , pale mtu anavyoona
hakutendewa ndivyo sivyo basi tufuate mkondo wa sheria na baadhi yao
mnaowasema walikuja hapa kwenye maadili wakasiliza wakawa cleared
wakaonekana hawana makosa.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni