Msanii Belle 9 amesema moja ya wasanii asiyowaelewa katika Bongo Flava ni Madee.
Muimbaji huyo akipiga stori na JJ wa Jembe FM amesema kuwa kutokana
anasikiliza wachanaji wengi wanaofanya vizuri anahisi kuna kitu
anakikosa kutoka kwa Madee.
“Honesty, let me be honesty, Madee huwa simuelewi. I don’t know, ujue
kuna wasanii inafika kipindi unasikiliza unasema huyo mtu ana-release
beat sio wimbo tena,” amesema.
“Labda kwa vile nasikiliza rappers ambao wanajua sana au kuna kitu
nakitegemea kutoka kwake kutokana muda mrefu yupo kwenye game, kuna kitu
nakimisi, so naona kama nikimsiliza na lose,” amesisiza.
Belle 9 ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa
jina la Dada, ameongeza kuwa mara nyingi ni vigumu mtu anayetoa kauli
kama yake kueleweka ila yeye amesema kile ambacho anaona kipo sawa na
kuwataka mashabiki wa Madee kuchukulia kawaida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni