June 10 2018 ameonekana akiwasili nchini Italia kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya na kukamilisha usajili wake katika club ya Sampdoria ya Ligi Kuu Italia Serie A, Colley ambaye amekuwa akiunda safu nzuri ya ulinzi ya Genk inadaiwa uhamisho wake wa kujiunga na Sampdoria utakamilika ndani ya saa 48 kutokea sasa.
Colley atauzwa kwa kiasi kinachoanzia euro milioni 6-8 kutoka Genk kwenda Sampdoria, Genk wanahitaji euro milioni 8 wakati Sampdoria wakifikia euro milioni 6, kama utakuwa unakumbuka vizuri Omar Colley na Mbwana Samatta ambao wamekuwa wakicheza Genk pamoja kwa miaka miwili sasa, wamekuwa na uhusiano mzuri, kiasi cha kuonekana sehemu mbalimbali wakiwa pamoja.
Hata hivyo Omar Colley ambaye ana mkataba na Genk wenye kipengele cha kuongeza miaka miwili zaidi, ameonesha dhamira ya dhati ya kuhitaji kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, ripoti zaidi zinaeleza kuwa Genk na Sampdoria wamefikia makubaliano na kutaka kuwekwa kipengeleza cha kufaidika kwa asilimia flani kwa mauzo ya Omar Colley kama akiuzwa kutoka Sampdoria kwenda timu nyingine.
Omar Colley ni room mate wa Mbwana Samatta kitu ambacho kimewafanya wawe karibu kwa kiasi kikubwa, Samatta na Colley hivi karibuni pia walionekana Macca Saudi Arabia wakiwa pamoja katika ibada ya umrah, fahamu kuwa sio Sampdoria pekee walionesha nia ya kumuhitaji Colley bali hata vilabu vya Everton, Hull Cit, Monaco na Hamburg ambavyo na vyenyewe vilikuwa vikihitaji huduma ya Colley.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni