Tuzo za Simba Mo Awards zinafanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo zitakuwa maalum kwa watu wa klabu hiyo waliofanikisha Simba kufanya vizuri kwa msimu wa 2017/18.
Wanachama,
viongozi, mashabiki na matawi ya klabu hiyo yatahusishwa katika
ugawajwi wa tuzo hizo zitazofanyika leo kuanzia saa 12 kamili jioni.
Kwa
mujibu wa mwanzilishi ambaye ni mwekezaji mpya wa klabu hiyo, Mohammed
Dewji 'Mo', amesema lengo mahususi la kuanzisha tuzo hizo ni kutambua
mchango wa waliofanikisha Simba kufikia hapo ilipo.
Baadhi
ya vipengele ambavyo vitakuwepo katika ugawajwi wa tuzo hizo ni
mchezaji bora wa mwaka, kiungo, mshambuliaji, shabiki na zinginezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni