Jumatano, 6 Juni 2018

Mchugaji Auawa kwa kushambuliwa na Mamba akibatiza


Habari kutoka Kusini mwa Ethiopia zinasema kwamba mchungaji ambaye alikuwa akiendesha ibaada ya kubatiza waumini ufukweni mwa ziwa amefariki baada ya kushambuliwa na mamba wakati akibatiza.

Mchungaji huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Docho Eshete alikuwa akiendesha ibaada hiyo ya waumini 80 siku ya Jumapili iliyopita katika ufukwe wa Ziwa Abaya katika mji wa Arba Minch wilaya ya Merkeb Tabya.

Wakazi wa mji huo waliliambia shirika la utangazaji la BBC kwamba Mamba huyo aliruka kutoka ndani ya maji wakati mchungaji huyo akiwabatiza waumini na kumng'ata miguu,mgongo na mikono majeraha yaliyosababisha kifo chake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni