Jumatano, 6 Juni 2018

MASOUD DJUMA AELEZEA MAHUSIANO YAKE NA KOCHA LECHANTRE, WANA UGOMVI? JIBU HILI HAPA



 Baada ya kuenea uvumi kuhusiana na kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, kuelezwa kuwa anataka kuondoka klabuni hapo na baadaye akaibuka kukanusha uwepo wa taarifa hizo, Djuma amefafanua namna mahusiano yake na kocha mkuu, Pierre Lechantre namna yalivyo.

Wakati Djuma akiwasili Simba kuanza kukinoa kikosi hicho ikiwa ni mapema baada ya Joseph Omog kuondoka, alikiongoza kikosi huku akionekana kusimama kila wakati kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo dhidi ya timu pinzani ukiendelea.

Kumekuwa kunaelezwa kuwa kitendo cha kocha huyo kuacha kufanya hivyo kwa mechi za hivi karibuni hivi kuwa ni ishara ya kutokuelewana na Mfaransa, Lechantre.

Kutokana na kuelezwa kwa tetesi hizo, Djuma amefunguka na kusema kutokuelewana kazini ni jambo la kawaida na haina maana kwamba kunakuwa na ugomvi ambao unaweza sababisha kufanya maamuzi ambayo si sahihi.

Kwa mujibu wa Radio EFM, Kocha huyo Mrundi amefafanua kitendo chake cha kuacha kusimama kwenye benchi la ufundi wakati mchezo ukiendelea kama ilivyokuwa zamani, haina uhusiano wowote na mahusiano mabaya na Lechantre kama wengi wanavyodai.

Djuma ameeleza kuwa yeye bado yupo Simba na ataendelea kuwepo mpaka pale mkataba wake utakapomalizika.

Ikumbukwe Djuma alipowasili Simba alitia kandarasi ya miaka miwili hivyo bado kibarua chake hakijafikia ukingoni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni