Jumatano, 6 Juni 2018

SIMBA KUNOA SILAHA ZAKE LEO KWA KAZI MAALUM YA KAKAMEGA KESHO


Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi leo mjini Nakuru, Kenya kwa ajili ya kukipiga na Kakamega HomeBoys kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano ya SportPesa Super Cup kesho.

Simba watakuwa wanacheza na timu hiyo ambayo iliiondoa Yanga katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo, Juni 3 2018 kwa ushindi wa mabao 3-1.

Wakati huo Simba nao walifuzu kufika hatua hiyo baada ya kuifungashia virago Kariobag Sharks FC ya Kenya kwa changamoto ya mikwaju ya paneati 3-2.

Mshindi wa mechi hiyo atatinga moja kwa moja mpaka fainali huku mchezo mwingine baina ya Singida United dhidi ya Gor Mahia FC ukisubiriwa.

Mechi dhidi ya Kakamega itaanza majira ya saa 9 kamili mchana na ikipigwa kwenye Uwanja uleule wa Afraha.

Bingwa wa michuano hiyo atapata nafasi ya kuelekea England kwenda kuiwakilisha Afrika Mashariki kucheza na Everton inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo katika Uwanja wake wa nyumbani, Goodison Park.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni