Kikosi cha Simba kimeapa kubadilika katika mechi yake ijayo ya michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup.
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema wanaamini hawakucheza katika mechi yao iliyopita ya michuano hiyo mjini Nakuru.
"Tulicheza
vibaya, kila mmoja wetu ameliona hilo. Hatuwezi kurejea tena kwa akili
hiyo. Wachezaji wote wameona tunahitaji kubadilika kwenye mechi ya
mwisho," alisema Djuma.
Simba
imevuka hadi nusu fainali kwa kuichapa Kariobang Sharks kwa mabao 3-2
ya mikwaju ya penalti lakini ilishindwa kuonyesha soka safi katika
dakika 90.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni