Mama Hamissa ameamua kuyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema..>>>”Mmenitukania Mwanangu hadi Tumbo la Uzazi limeniuma 😔😔 , natamani ningewazaa wawili ili Ajifariji kwa mwenzie.
“Pia ningeomba familia zote zilizopo Instagram , Mpunguzieni matusi na kumdharilisha Mwanangu , kama kawakosea ninamwombea Msamaha mwezi huu mtukufu . .
Mpeni Amani ili na mimi nifurahie furaha ya Uzazi wangu . Ni mwenyezi Mungu pekee huchagua barabara atakayopitia Mwanaadamu.” – Mama Hamissa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni